Lionel Messi ameiambia Barcelona anataka kuondoka klabu hiyo mara moja huku Manchester City ikiongoza katika kinyang’anyiro cha kumwania mshambuliaji huyo, 33, wa Argentina. (Esporte Interativo, via Mirror)
Barcelona itasikiliza ofa za mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, 29, mwaka mmoja tu baada ya kuwasili kutoka Atletico Madrid kwa pauni milioni 107. (Sport via Express)
Mchezaji wa Bayern Munich Thiago Alcantara amekubalia mkataba wa miaka minne na Liverpool, huku klabu ya Bundesliga ikitaka ziada ya pauni milioni 30 kwa kiungo huyo wa kati, 29, raia wa Uhispania. (RMC Sport, via Mirror)
Arsenal imefikia makubaliano na nahodha Pierre-Emerick Aubameyang, 31, juu ya mkataba mpya na pia inafuatilia kwa karibu kumsaini mlinzi wa Brazil Gabriel Magalhaes, 22, kutoka Lille. (Telegraph)
Mabingwa wa Serie A wanawafuatilia kwa karibu kutaka kuwasajili mshambuliaji wa Arsenal raia wa Ufaransa Alexandre Lacazette au mshambuliaji wa Wolves raia wa Mexico Raul Jimenez, ambao wote wana umri wa miaka 29. (Sky Sports)
Juventus iko tayari kumuuza Paulo Dybala,26, na Manchester United – na Tottenham zimeonesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo wa Argentina. (Gazetta Dello Sport – in Italian)
Leicester inakabiliana na ushindani kutoka kwa Paris St-Germain katika kumwania beki wa Atalanta na Ubelgiji Timothy Castagne, 24. (Calciomercato via Leicestershire Mercury)
Inter Milan inamnyatia mlinzi wa Manchester United Chris Smalling, 30, na huenda ikalipa kitita cha pauni milioni 20 kwa ajili ya mchezaji huyo aliyekuwa beki wa kati wa England. (Metro)
Macho ya Leeds United sasa yapo kwa mlinzi wa Ujerumani na Freiburg Robin Koch, 24, huku matumaini ya kufikia makubaliano na ambaye alikuwa mlengwa wao mkuu, beki wa kati wa Brighton Ben White, 22, yakionekana kudidimia. (Telegraph – subscription required)
Kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa wa timu ya vijana walio chini ya miaka -19 Aliou Traore, 19, yuko tayari kujiunga na Caen kwa mkopo. (Goal)
Meneja wa zamani wa Bournemouth Eddie Howe, mwenye umri wa miaka 42, hapangi kurudi katika soka hadi Krismasi ambapo atakua amepumzika baada ya kuondoka katika the Cherries. (Mail on Sunday
Kocha wa Barcelona Quique Setien anatarajiwa kupigwa kalamu leo Jumatatu huku kocha wa Uholanzi Ronald Koeman akiangaziwa kama mwenye uwezekano wa kuchukua nafasi yake amesema Guillem Balague.
Barcelona ya La Liga iliyokuwa ya pili ilicharazwa mabao 8 dhidi ya 2 na Bayern Munich wakati wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ijumaa.
Sevilla ilididimiza matumaini ya Manchester United ya kumaliza msimu kwa kishindo wakati wa mchuano wa nusu fainali ya Ligi ya Europa huko Cologne.
Timu ya Ole Gunnar Solskjaer ilipoteza katika nusu fainali ya tatu msimu huu licha ya kuchukua uongozi pale Bruno Fernandes alipofunga penalti yao ya 22 msimu huu baada ya Marcus Rashford kuchezewa faulu na Diego Carlos.
Borussia Monchengladbach wanapanga uhamisho wa kiungo wa safu ya mashambulizi wa timu ya Ufaransa Lyon Maxwel Cornet, ambaye alifunga bao la kwanza Katika Ushindi wao wa mechi ya kwanza ya Ligi ya Championi dhidi Manchester City, lakini rais huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 23 pia anasakwa na klabu ya Wolfsburg. (Le 10 Sport, in French)
Kiungo wa kati Jeff Hendrick yuko tayari kusiani mkataba na Newcastle United kwa uhamisho wa bila malipo. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 28 kutoka Jamuhuri ya Ireland anayechezea timu ya Burnley baada ya mkutaba wake Turf Moor kumalizika tarehe 30 Juni. (Talksport)
Newcastle Pia wanamtaka difenda wa Oxford United na nahodha Rob Dickie, mwenye umri wa miaka 24. (Sun on Sunda
More Stories
15 wajinoa Juventus,akiwemo mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mbeya
Za Kwetu Fashion Show, yawapaisha wanamitindo nchini
TCAA yaadhimisha siku ya usafiri wa anga Duniani kwa kushiriki mbio za Marathon UDSM