December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tetesi za soka Ulaya

Meneja mpya wa klabu ya Barcelona Ronald Koeman amemfanya mshambuliaji wa Misri Mohammed Salah kuwa mchezaji anayemlenga sana msimu huu. (Sunday Express)

MO Salah

Manchester United huenda ikawasilisha ombi la kumsajili winga wa Real Madrid na Wales Gareth Bale kama mbadala wa winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 20. (Sunday Express)

Beki wa kushoto wa Uhispania Sergio Reguilon, 23, angependelea kuhamia kwa mkopo katika klabu ya Sevilla badala ya kuhamia Manchester United. (AS – in Spanish)

Ombi laTottenham kumsajili mshambuliaji wa Itali na Torino Andrea Beloti lakataliwa. (Sky Italia – in Italian)

Gareth Bale

Manchester United imejiandaa kumlipia beki wa Monaco na Ufaransa Benoit Badiashile 19 dau la £23m. (L’Equipe, via Sunday Express)

Meneja wa klabu ya Inter Milan Antonio Conte anataka kumleta katika klabu hiyo beki wa kushoto wa Chelsea na Uhispania Marcos Alonso, 29, katika ligi hiyo ya Seria A.. (Sky Italia, via Mail on Sunday)

Tottenham inaandaa kuwasilisha ombi la kumnunua mshambuliaji wa Braga na Portugal Paulinho, 27. (90min)

Manchester City na kiungo wa kati wa Ukraine Oleksandr Zinchenko, 23, yuko tayari kuwa miongoni mwa makubaliano ya kubadilishana wachezaji kwa beki wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly, 29. (Radio Marte, via Sun)

Paulinyo

Kiungo wa kati wa zamani wa Manchester City na Ivory Coast Yaya Toure, 37, hana mpango wa kustaafu na sasa anataka kucheza katika ligi ya Serie A . Kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuondoka katika klabu ya China Qingdao Huanghai in January. (Tuttomercato via Goal)

West Ham inamnyatia winga wa Brighton na England mwenye umri wa miaka 26 Solly March na wameanza mazungumzo. (90min)

Mshambuliaji wa Dijon na Ufaransa Mounir Chouiar, 21, analengwa na klabu ya Leeds, Wolves na Arsenal. (France Football – in French)

Leeds inataka kumnunua kiungo wa kati wa Chelsea na England Conor Gallagher, 20. (Mail on Sunday)

Ombi la Aston Villa la kumnunua mshambuliaji wa Burkina fasso na Lyon Bertrand Traore kwa dau la 15.7m lagonga mwamba ;. (Footmercato – in French)

Betrand Traore

Klabu ya Burnely itawasilisha dau la £8m kumnunua mshambuliaji wa klabu ya Mainz na Sweden Robin Quaison, 26. (Mail on Sunday)

Liverpool imekubali makubaliano ya £1.8m kumnunua kipa wa Fluminense 17 raia wa Brazili Marcelo Pitaluga. (Globo Esporte, via Mail on Sunday)

Sunderland imeshinda kinyang’anyiro cha kumsaini kiungo wa kati wa Hartlepool Josh Hawkes. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 pia analengwa na klabu za Leeds, Newcastle na Middlesbrough. (Team Talk)