Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online
KATIKA kuadhimisha siku ya Mtandao kwa mwaka 2022 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeendelea kusisitiza na kuwaonya watu wasio wema ambao wamekuwa wakitumia mtandao kuwalaghai vijana na kupelekea kusababisha athari mbalimbali za kiusalama ikiwemo taarifa zao kuonekana na kutumiwa vibaya dhidi yao.
Akizungumza katika maadhimisho hayo yaliofanyika Jijini Dar es salaam kwa niaba ya Mkurungezi Mkuu (TCRA) Dkt Jabir Bakari , Mkurugenzi wa leseni na ufatiliaji ( TCRA) John Daffa amesema uwezo wa mtandao kuficha utambulisho wa mtumiaji, umewawezesha watu wenye nia ovu kujifanya kama vijana wadogo na kushawushi vijana kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi katika umri mdogo.
Amesema watu hao wamekuwa wanaweza kuiba au kukushawishi uwatumie tariffs yako binafsi kama pichai, nywila, mwaka wa kuzaliwa nk na kuzitumia kufanya uhalifu mtandaoni ikiwa ni pamoja kufanya utapeli, kusambaza taarifa za uongo wakilenga kuchafua taswira yako au kufanya manyanyaso dhidi yako na kusababisha usumbufu kwa waathirika wa vitendo hivi.
“Pamoja na mitandao ya kijamii kuwa nyenzo za kulinda usiri vijana wengi hawatumii nyenzo hiyo na hivyo kusababisha taarifa zao kuonekana kwa watu wenye nia mbaya na hivyo kuzitumia vibaya dhidi yao”amesema Daffa
Akizungumzia kuhusu takwimu amesema hadi Disemba mwaka Jana idadi ya watumiaji wa mtandao wa intaneti imekuwa hadi kufikia watu million 29.3 wakati Tanzania ikiendelea kuwa nchi ambayo wanapata wananchi wake wanapata huduma mbalimbali za Mawasiliano kwa gharama snafu ikilinganishwa na nchi nyingi duniani.
Alibainisha kuwa serikali imejipanga vyema kuandaa mazingira bora na wezeshi kwa jamii ya watanzania kushiriki ipaswavyo kwenye uchumi wa kidijitali.
” Tumeshuhudia watu wengi wakiinuka kiuchumi kwa kutumia mtandao. Wengi wanaweza kufanya biashara na kuinua maisha yao wenyewe na wale waliowaajiri ikiwa ni pamoja na kuchangia kwenye pato la taarifa,’amesema
Naye Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ( Tehama), Connie Francis amesema Tanzania ni moja ya nchi iliyochukua hatua katika matumizi ya tehama.
Alisema Maadhimisho ya Siku hii ni mpango wa kimataifa ulioanzishwa 2014 kwa lengo la kuhamasisha matumizi bora na salama ya mtandao wa intaneti.
Husna Ramadhani kutoka shule ya Sekondari Changombe Demonstration ni miongoni mwa wanafunzi walioshiriki katika maadhimisho hayo amesema yeye kama mwanafunzi amekuwa akituambia matumizi ya Mtandao kwa ajili ya kujisomea na kumpa fursa ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu elimu.
Akizungumzia kuhusu manyanyaso ya mtandaoni aliiomba Serikali kuweka sheria kali itakayosaidia kukomesha vitendo hivyo.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato