TNa Mwandishi wetu, Timesmajira
MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imeibuka mshindi wa tatu kwa upande wa Mamlaka za Udhibiti katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2023 (Best Presented Financial Statements for the Year 2023 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania(NBAA).
Katika hafla hiyo iliyofanyika Novemba 29,2024 katika Hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Katika tuzo hizo Mshindi wa kwanza amekuwa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imeibuka mshindi wa pili.
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Uongozaji Ndege katika Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA),Flora Alphonce ameongoza ujumbe wa TCAA katika upokeaji wa tuzo hiyo.
More Stories
Dkt. Mpango aipongeza CRDB kuzindua Samia Infrastructure Bond, Kukusanya Bilioni 150 kwa Ujenzi wa Barabara za Mijini na Vijijini
Waajiri wahimizwa kuzingatia misingi ya utu na umakini kazini
FCC yazindua wiki ya ushindani kitaifa