Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema katika mwaka 2022/23 TCAA ilipata alama za juu katika udhibiti wa sekta ndogo ya Usafiri wa Anga, ambapo TCAA ilipatiwa tuzo yenye jumla ya Dola za Marekani 1,000,000 na Shirika la Usafiri wa Anga Duniani kwa ajili ya kuendelea kuimarisha udhibiti wa usafiri wa anga.
Amesema Fedha hizo za tuzo pamoja na mambo mengine, zitasaidia kugharamia mafunzo kwa walengwa 170.
Prof. Mbarawa ameyasema hayo leo wakati akiwasilisha Bungeni mpango wa Makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka wa fedha 2023/24 ambapo amesema Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imekuwa ikikaguliwa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) kulingana na masharti na viwango vya Shirika hilo.
“Mafunzo hayo yanatolewa ndani na nje ya Tanzania katika fani za ukaguzi na utoaji huduma za Usafiri wa Anga; Uchunguzi wa ajali za ndege; Uhandisi wa miundombinu ya viwanja vya ndege; Utoaji wa huduma za ndege (Operators).”
Pamoja na mambo Mengine, Prof. Mbarawa amesema Wizara kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imeendelea kutoa huduma za udhibiti wa usafiri wa anga, viwanja vya ndege, masuala ya kiusalama na kiuchumi katika huduma za usafiri wa anga pamoja na kutoa huduma za uongozaji ndege katika viwanja 14 vya Dar es Salaam, Zanzibar, Mwanza, Arusha, Pemba, Tabora, Kigoma, Dodoma, Iringa, Songwe, Mtwara, Tanga, Songea na Kilimanjaro.
More Stories
Nani kuwa mrithi wa Kinana CCM?
Watendaji Songwe wapatiwa mafunzo uboreshaji daftari la mpiga kura
Samia: Mwaka 2024 ulikuwa wa mafanikio