March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TBL yafanya maadhimisho ya  siku ya Global Beer Responsible

 

Na Mwandishi wetu,Timesmajira 

Kampuni ya bia Tanzania Breweries Plc (TBL),  imefanya maadhimisho ya siku ya  Global Responsible Beer Day katika mikoa minne nchini kwa lengo la kuihamasisha jamii juu ya umuhimu wa unywaji wa pombe kwa uwajibikaji.

Akizungumza leo  wakati wa maadhimisho hayo, Neema Temba, Mkurugenzi wa Masuala ya Sheria na Mahusiano wa TBL, amesema maadhimisho haya ni sehemu ya juhudi endelevu za AB InBev na TBL katika kuimarisha utamaduni wa unywaji kwa kuwajibika, kuelimisha jamii kuhusu madhara ya unywaji kupita kiasi, na kuchochea mabadiliko chanya ya kitabia kupitia kampeni mbalimbali za uhamasishaji. 

 “Sisi kama wazalishaji wa bia hapa nchini tuna wajibu wa kuikumbusha jamii yetu, hasa wateja wetu wanaofurahia bidhaa zetu, kuhakikisha wanakunywa kistaarabu na kwa kuwajibika. Tunataka kuona jamii inayofurahia bia zetu kwa usalama, bila madhara kwao au wengine.

” kupitia kampeni ya “Kunywa Mdogo Mdogo”, TBL inahamasisha watumiaji wa vinywaji vyao kufuata vidokezo vifuatavyo:

Kunywa maji ya kutosha wakati wa kufurahia bia,Kula chakula kabla na baada ya unywaji wa pombe na Kuepuka kuendesha gari endapo umelewa,”amesema.

Aidha ametaja  mikoa ambayo wameadhimisha siku hiyo ni pamoja na Mwanza, Mbeya, Arusha na Dar es salaam. 

Amesisitiza kuwa Kwa mujibu wa TBL, dhamira pana ya kampuni yao ni  kuhakikisha wateja wake wanafanya maamuzi sahihi kuhusu matumizi ya pombe, huku ikiunga mkono jitihada za serikali na wadau wengine katika kupambana na unywaji kupita kiasi.