Na Bakari Lulela, TimesMajira Online
SERIKALI ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, imeupongeza uongozi wa tawi la amana Ilala jijini Dar es salaam kwa kuandaa mafunzo elekezi yenye kuwajengea uwezo wajumbe walioko katika maeneo hayo.
Mafunzo hayo yalikuwa na lengo la kuwaelimisha viongozi hao kuweza kutambua majukumu ya kazi zao wanapokuwa wakiwatumikia wananchi.
Akizungumza jijini Dar es salaam, mwenyekiti wa chama cha Mapindizi (CCM) Said Side amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa mabalozi kutambua mipaka ya majukumu yao.
“Mafunzo haya ni muhimu kwa wajumbe wakati ambapo tunajiandaa kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa hivyo wapate kuwaeleza wananchi mambo ambavyo Serikali ya CCM imekuwa imiyafanya,” amesema Side
Aidha mwenyekiti huyo amewataka wajumbe hao kutumia elimu hiyo kama nembo ya kukielezea chama cha CCM kwa wanachama wake na wananchi kwa ujumla .
Kwa upande wake Naibu spika na Mbunge wa Ilala Iddi Azan Zungu amesema wajumbe wote waliopata mafunzo waweze kumtangaza vema Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan dhidi ya kazi alizokuwa amezifanya.
Mbunge huyo ameeleza na kuzitaja miongoni mwa kazi hizo ni pamoja na ujenzi wa barabara za mitaa , ujenzi wa miundo mbinu ya shule ,masoko na masoko pamoja na utoaji wa mikopo wezeshi .
Nae Mwenyekiti wa tawi la amana Balozi Kindamba ameeleza kuwa mafunzo hayo yatawawezesha wajumbe hao kutambua mipaka ya kazi zao katika kukielezea chama cha mapindizi CCM kwa wanachama na wananchi .
More Stories
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito