Na Jackline Martin, TimesMajira Online
KAMPUNI ya michezo ya kubahatisha, Tatu mzuka imezindua rasmi kampeni ya “Bosi Karudi” yenye lengo la kumfanya mtanzania aweze kunufaika na milioni 300 ambazo zilikua zikitolewa hapo awali huku wakiwahakikishia wachezaji wote usalama wa pesa zao.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Meneja wa Masoko kutoka Tatu Mzuka, Jackline Kaboko alisema yale madau makubwa yaliyokuwa yakitoka zamani kwa sasa wanayatoa tena kwa kupitia droo za kila dakika 5 lakini pia droo ya Jackpot mbili kubwa.
“Mtanzania anaweza kushinda kuanzia laki mbili mpaka milioni 6 kupitia droo ya kila dakika 5, lakini pia siku ya jumatano tutakuwa na jackpot ya milioni 20 itakayoenda kwa watanzania watakaobahatika.
“Pia kuna bidhaa mbalimbali kama vile bodaboda, bajaji, smartphones, laptops n.k, pia kuna jackpot ya jumamosi ambapo tunatoa milioni 50 kwenda kwa watanzania ambao wamebahatika”
“Jinsi ya kucheza unabonyeza menu ya malipo ya mtandao wako wowote unaoutumia kisha kwenye namba ya kampuni ni 555111 na kumbukumbu namba unaweka namba zako tatu za bahati ambazo ni zozote kuanzia namba 0-9 na kiasi ni kuanzia shilingi 1000- 30,000,” alisema Kaboko.
Aidha alisema dhumuni la kutoa pesa hizo ni kuhakikisha kwamba wanayainua maisha ya watanzania kwenye nyanja ya uchumi.
Kuhusu usalama wa pesa za wachezaji, alisema Tatu mzuka ipo chini ya usimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania (GBT), ambapo wanaratibiwa kuhakikisha pesa anayocheza na pale atakaposhinda pesa zake atazipata bila kuzurumiwa.
“Kuna ile hali ya kwamba matapeli wanakupigia wanakwambia umeshinda pesa na kutakiwa utume ela kwenye simu ukishinda hautatakiwa kutuma kiasi chochote cha pesa, sisi ndiyo tutakupigia na kukukabidhi zawadi zako,” alisema.
Kwa upande wake Balozi wa Kampuni hiyo, Geah Habibu alisema msimu huu mshindi atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 1 kila siku, kasoro siku ya jumatano na jumamosi ambazo ndio siku za jackpot kubwa.
Naye Zai kijiwe Nongwa ambaye ndiye atakuwa mgeni rasmi wa mamilionea wa jumamosi aliwasihi watanzania wote kucheza na Tatu mzuka ili kuweza kujipatia ushindi na kujiinua kiuchumi.
More Stories
DC Korogwe awataka viongozi wa vijiji kuwatumikia wananchi kwa uadilifu
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam