November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TASAF yamkomboa mlemavu aliyeishi chini ya mti na familia yake

Na Esther Macha, TimesMajira, Online, Busokelo

FURAHA Mwamasika ni mkazi wa Kikuba katika halmashauri ya Busokelomkoani Mbeya ambaye ni mlemavu wa viungo ambaye alilazimika kuishichini ya mti na watoto wake saba (7) kutokana na nyumba aliyokuwaakiishi kusombwa na mafuriko hivyo maisha yake kuhamishia kwenye mtilicha ya mvua kunyesha .

Mwamasika amesema hayo leo alipotembelewa na waandishi wa habariwaliofika kijijini hapo kwa lengo la kuangalia jinsi wanufaika wampango wa kunusuru kaya maskini wanavyoondokana na umaskini na maishamagumu kupitia mpango huo.

Mwamasika amesema kuwa walikuwa na maisha magumu hali ambayoiliwafanya kushindwa kupata chakula na hata watoto kushindwa kumudumasomo kutokana na ukosefu wa sare za shule na mahitaji mengine muhimu.

Amesema kuwa hawakuwa na njia nyingine baada ya nyumba yao nyasikusobwa na mafuriko hivyo kulazimika kuishi chini ya mti wa Muembena familia yake ya watoto saba hali ambayo ilipelekea maisha kuwamagumu katika familia hiyo.

“Sikuwepo kwenye mkutano wa kijiji kuja kuangalia maisha niliyokuwanikachaguliwa kuingia kwenye TASAF kutokana na kuwa shida kwelitulikuwa tunalala nje na watoto ,kweli ikabidi zije hela ikabiditununue nguruwe wawili tukafuga wakakua tukauza na kufyatua tofari nakuanza ujenzi ndiko tunaishi mpaka sasa mi watoto wangu “amesema Mwamasika.

Hata hivyo Mwamasika amesema kuwa bado mfuko huo unaendelea kuwasaidia kwani ana watoto wanaosoma kupitia mpango wa huo na kusema bila TASAFmaisha yalikuwa magumu sana .

“Nilipata ulemavu huu baada ya kujikwaa t undo ulemavu huu nilionasifanyi chochote cha uzalishaji ,fedha hii ya TASAF imenisaidiakupata matibabu hivyo ninawaasa ndugu zangu ambao ni wanufaika wamfuko wa TASAF fedha wanazopewa kuzitumia vizuri kwa malengo yakujiendeleza “amesema Mwamasika.

Witnes Mwamasika ni Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Lufyilo amesemakuwa mpango wa huo wa kunusuru kaya maskini umewasaidia katika maishayao kutoka kwenye umaskini ,na kusema kuwa kabla ya kuingia kwenyempango walikuwa wakiishi maisha ya magumu mfano kutokuwa na mavazi,kutokuwa na uhakika wa kutopata mlo .

“Mpango huu ulivyoanzishwa umeanza kuinua maisha yao yamekuwa tofautikwani hivi sasa mfuko huo umeweza kuwasaidia mahitaji ya shule“amesema .

Rehema Michael ni mmoja wa wana familia wa Mzee Mwamasika amesema kuwawatoto wake kabla ya kuingia kwenye walikuwa wanashindwa kupatamahitaji ya shule na hata kushindwa kwenda shule kutokana na kukosavifaa vya shule .

Aidha Rehema alimuomba Raisa Samia Suluhu Hassan kutowasahau kwenyempango huo ambao umekuwa mkombozi kwa kaya maskini kwani ni farajakwa kaya zisizo jiweza kimaisha.

“Kama hivi sasa Mimi mume waqngu alijikwaa tu miaka mitatu iliyopitalakini mpaka sasa ni mlemavu wa kudumu ila nashukuru uwepo wa TASAFkwani ndo imenifikisha hapa hata mume wangu alipopata shida hii yakujikwaa na kupata ulemavu fedha za TASAF ndizo zimemfikisha hapoalipo”amesema .

Mratibu wa shughuli za TASAF halmashauri ya Busokelo ,Geofrey Mwaijele amesema kuwa kiijiji cha Mbambo kata ya Kambasegera kinawalengwa 104 ambao wamehusika katika kutekeleza ajira za muda namfereji huo una mita 314 kutoka kwenye chanzo.

Mwaijele amesema kiasi kilichotumika katika ujenzi wa mfereji huomil.6 kwa mita 150.6 ambazo zimeweza kujengwa na mfereji huo umewezakuwanufaisha walengwa kwa maana kwamba wanalima mashamba ya mahindi mboga mboga ambazo mwisho wa siku wanapeleka sokono kwa lengo lkuongeza kipato katika kaya ukiachana na fedha ambazo wanawezeshwa naTASAF lengo kuu ni kuongeza kipato kwa njia ya kilimo cha umwagiliaji.