November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TASAF yamjengea nyumba ya bati Fransiska Paskali

Na Sophia Fundi, Timesmajira, Karatu

MFUKO wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), umemsaidia mama mwenye familia ya watu saba, Fransiska Paskali kutoka kijiji cha Qaru wilayani Karatu, kumilili nyumba ya batu yenye vyumba vitatu .

Mama huyo ambaye hakuwa na chochote kabla ya kuingizwa kwenye mfuko mwaka 2014, huku akikosa milo mitatu kwa siku pamoja kushindia uji yeye na familia kutokana na ukata aliokuwa nao.

Mara baada ya kuingizwa kwenye mfuko huo, ameishukuru serikali kuziona kaya masikini na kuwapatia ruzuku kwa ajili ya kujikimu kimaisha.

Akielezea maisha yake, Fransiska amesema wakati mfuko unaanzishwa alipokea shilingi 44,000, jambo ambalo hakuamini kwani alikuwa hana chochote katika familia yake.

Flansiska amesema, alipokea kiasi hicho kwa miezi miwili lakini hakuweka akiba zaidi ya kununua mahindi kwa ajili ya chakula na kulipia mahitaji ya watoto shuleni.

Amesema, alianza kuweka akiba alipopokea ruzuku ya awamu ya tatu ambapo wakati huo ruzuku ilipanda na kufikia 58,000, ndipo alipoanza kuweka kiasi cha shilingi 20,000 kila anapopokea ruzuku na kuanza kununua ng’ombe wawili, kondoo watatu na kuku mmoja.

Mifugo hiyo kwa sasa imefikia, ng’ombe wapo wanne, kondoo 18 na kuku zaidi ya wanane, ambao wamekuwa msaada kwake kwani amekuwa akiwauza na kununua bati kwa ajili ya kuezekea nyumba ambayo kwa sasa anaishi na familia yake.

Amewaomba wanufaika wa TASAF, kutumia ruzuku wanayoipata kwa malengo yaliokusudiwa na kuweka akiba itakayowasaidia katika kuinua kipato.