November 8, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TASAF inavyoboresha maisha ya wananchi

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

MKURUGENZI  wa mawasiliano na Mfumo wa Mfuko wa  Kunusuru Kaya masikini (TASAF)  Japhet Boazi amesema mfuko huo unaendelea kutekeleza lengo la kuanzishwa kwake la kusaidia wananchi na kuwatoa katika umasikini.

Boaz ameyasema hayo  Juni 19,2024  katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Nchini yanayofanyika jijini Dodoma. 

 “Kama lilivyo lengo la TASAF katika kunusuru kaya masikini ,tunaendelea kutekeleza jukumu hilo kwa  kuzipatia ruzuku kaya za walengwa ili ziweze kuboresha hali zao za maisha kwa na  kuwekeza katika shughuli za uzalishaji mali.

Amesema hatua hiyo inakwenda kuziongezea kaya hizo kipato ambapo kinawasaidia   kumudu mahitaji yao muhimu ikiwemo Afya, Lishe, Elimu na kuwasaidia kuondokana na  umasikini katika kaya hizo.

Kwa mujibu wa Boaz,ASAF imekuwa ikisaidia kaya maskini kwa kuwapa mitaji na mafunzo mbalimbali kama ya ujasiriamali ili waweze kusimama na kujitegemea wenyewepindi  wanapofanikiwa .

Amesema Mpango wa TASAF umeleta mabadiliko makubwa katika jamii na kwamba  wanufaika wake ni wengi ambapo wamejikita  katika masuala ya ujasiriamali ikiwamo wa kilimo ufungaji na utengenezaji wa  bidhaa mbalimbali.

“Kwa hiyo hata katika wiki hii ya Utumishi wa umma ,tupo hapa kwenye maonesho kwa ajili ya kufikisha na kutoa elimu kwa wananchi lakini pia  kusikiliza malalamiko kwa  wenye changamoto mbalimbali kuhusu mfuko huo na kuwasaidia kuzitatua.

Mnufaika wa Mfuko Kuluthum Abdallah ameishukuru Serikali kupitia Mfuko huo huku akisema umekuwa mkombozi katika maisha yake.

“Naushukuru sana Mfuko wa TASAF ,umenipatia elimu na mtaji na kuniwezesha kuanzisha biashara yangu ambayo imeniwezesha kujitegemea kiuchumi.”amesema Kuluthum