December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TANZIA: RAIS MAGUFULI AMEFARIKI

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Dar es Salaam.

TUMEMPOTEZA kiongizi wetu shupavu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh. John Joseph Magufuli ambaye amefariki kwa maradhi ya moyo.

Akihutubia taifa makamu wa Rais mama Samia Lukuhu HAssan amesema kuwa marehemu alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa akipatiwa matibabu.

Amesema marehemu Rais Magufuli alilazwa Machi 6, 2021 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa tatizo la mfumo wa umeme.

Amesema Machi 7,mwaka huu, aliruhusiwa na kuondoka kuendelea na majukumu yake na Machi 14 alijisikia vibaya na kurudi hospitali ya Mzena ambako aliendelea na matibabu hadi umauti ulipomkuta.

Amesema nchi itakuwa na maombolezo ya siku 14.

Apumnzike kwa amani!