Hassan Nassor Moyo ambaye ni Mwanasiasa mkongwe na mwasisi wa Mapinduzi Zanzibar amefariki usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake mkoani Tanga
Mzee Moyo ambaye pia ni Waziri Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikuwa pia aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar
Mzee Moyo alikuwa mwanachama wa Chama cha Afro Shirazi (ASP) tangu kilipoanzishwa Februari 5, 1957 baadaye Februari 5, 1977 akajiunga na chama cha Mapinduzi akiwa na kadi namba 7.
Aidha Mzee Moyo ndiye alikuwa Mratibu Mkuu wa Maridhiano ya Zanzibar ya Novemba 5, 2009 yaliyowakutanisha Rais Mstaafu wa Zanzibar (awamu ya sita), Dk Aman Abeid Karume na Maaalim Seif Sharif Hamad katika kutafuta mbinu ya kuondoa tofauti iliyokuwepo kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010.
Mzee Hassan Nassor Moyo alivuliwa uanachama wa chama cha mapinduzi CCM, hatua iliyofikiwa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa wa Magharibi, Unguja viswani Zanzibar
More Stories
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam
DCEA na Shirika la Posta watiliana saini dhidi ya usafirishaki wa dawa za Kulevya
NHIF yarejesha Toto Afya Kadi ,yazindua vifurushi vipya