Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online
MWIGIZAJI mkongwe wa kikundi cha Maigizo kinachorusha mchezo wao wa kuchekesha wa Mizengwe kupitia Televisheni ya ITV, Jumanne Alela maarufu kama ‘Mzee Matata’ amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu tokea Juni 13, 2021 mwaka huu.
Taarifa ya kifo chake zimethibitishwa leo na mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya umma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha.
Aligaesha amesema, msanii huyo amefariki dunia jana saa tano na nusu, baada ya kulazwa katika hospitali hiyo
Kwa mujibu wa mwigizaji maarufu nchini, Madebelidai, mazishi ya Mzee Matata yatafanyika kesho kwenye Makaburi ya Buguruni,Malapa jijini Dar es salaam.
“Mazishi ya Mwanatasnia mwenzetu Mzee Jumanne Alela (Mzee Matata) yatafanyika kesho saa saba mchana kwenye Makaburi ya Buguruni-Malapa. Msiba upo kwa ndugu zake, Chamazi kwa Mkongo (jijini Dar),” imesema taarifa kutoka kwa Madebelidai.
More Stories
Mzee wa Bwax afunika ‘Kitaa food Fest’ Mbagala
TBL yazindua Kampeni ya ‘Smart Drinking’
Msimu wa nne,tuzo za eagle entertainment, kufanyika kivingine