Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amesema vifo vitokanavyo na UKIMWI vimepungua kwa 50% kutoka vifo 64,000 mwaka 2010 hadi 32,000 mwaka 2020.
“ Maambukizi mapya ya VVU kwa watu wazima (miaka 15 na zaidi) yameshuka kutoka 110,000 mwaka 2010 hadi 68,000 mwaka 2020; na Maambukizi mapya kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto (Mother to child transmission) yameshuka kutoka 18% mwaka 2010 hadi 7% mwaka 2020.”
Hayo yamesemwa na waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene kwenye harambee ya uchangishaji wa fedha za kupanda mlima kilimanjaro ili kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI mwaka 2022.
Alieleza Matumizi ya dawa za kufubaza VVU (ARV) kwa WAVIU wanaojua hali zao za maambukizi yameongezeka kutoka 95% mwaka 2016 hadi 98% mwaka 2020;
Aidha maambukizi mapya ya VVU kwa watu wazima (miaka 15 na zaidi) yameshuka kutoka 110,000 mwaka 2010 hadi 68,000 mwaka 2020.
“Serikali, tayari imetenga fedha Bilioni 1.88 kwenye bajeti ya 2022/2023 ili iendelee kuchangia AIDS TRUST FUND alisema waziri”
Amefafanua serikali itaendelea kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa afua zinazotekelezwa za Mwitikio wa VVU na UKIMWI zinaleta tija kwa makundi mbalimbali katika jamii.
Amesema ili kufikia malengo haya pamoja na mengine katika kuishinda vita hii dhidi ya VVU na UKIMWI, kunahitaji nguvu ya pamoja kati ya serikali na wadau wengine, hususan sekta binafsi ili kupata rasilimali fedha ya kutosha.
“Kili challenge inalenga kupunguza athari za kupungua kwa misaada ya wahisani na kuiwezesha Nchi kuimarisha uwezo wa ndani kwa ajili ya kudhibiti UKIMWI”
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Dkt. Leonard Maboko, amesema kutakuwa na wapanda baiskeli 28 kuuzunguka Mlima Kilimanjarao na wapandaji mlima kwa Mguu 24.
Kwa muda wa miaka 20 zoezi hili limekuwa likifanywa na kuchangia kiasi cha dola za kimarekani million 7 zimekusaywa na zimesaidia sana katika makabilia kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI mwaka.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Stephen Kagaigai, ameshukuru wadau wote walioshiriki kwa lango la kutafuta fedha za muitikio wa VVU na UKIMWI.
“Nimatumaini yangu kwamba ushirikiano huu utaendelea ili kufikia malengo ya sifuri tatu, kufikia mwaka 2030 ya kutokuwa na maambukizi mapya, unyanyapaa na vifo vitokanavyo na UKIMWI. Kushuka kwa maambukizi ya UKIMWI ni matokeo ya pamoja ya Wadau wa sekta ya Umma na Binafsi”
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania; Dkt. Leornad Maboko amesema fedha zinazopatikana katika harambee zitasaidia sana katika kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI.
“Tumeunda kill Trust Fund, wajumbe wa bodi wanatoka upande (GGM) Geita Gold Mine na wengine wanatoka Tume ya Kudhibiti na Kupambana na UKIMWI, bodi imesaidia sana katika kuja na mikakati ya kufanya mara baada ya kukusanya Fedha”
Naye Makamu wa Rais wa Kampuni ya Mgodi wa Geita Gold Mine Bwn. Simon Shayo, Makamu wa Rais wa Kampuni ya Mgodi wa Geita (GGM); amesema tumekuwa tukikusanya fedha zinazosaidia maeneo mabalimbali, baadhi ya taasisi zimeasisiwa kutokana na uwepo wa mfuko huo ikiwemo kituo cha kulelea Watoto yatima Mkoani Geita.
“Kituo kilianza na Watoto 13 lakini sasa kina Watoto zaidi ya 170 ambao wanapata elimu wanapata huduma za afya kutokana na watu wanajitolea kuchangia kupitia Mfuko. Kundi la kwanza la Watoto walioingia kwenye kituo hicho wengi wao wako chuo kikuu”
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini