

.
Na WMJJWM- New York Marekani
Serikali ya Tanzania imejidhatiti kuinua hadhi ya mwanamke kupitia ushirikiano baina yake na Serikali ya China hususani katika nyanja ya Tehama na Uchumi na hatimaye kuwa na Taifa lenye Usawa wa kijinsia.
Hayo yamebainishwa katika mazungumzo yaliyofanyika baina ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu na Mwakilishi wa Kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa ikiwa ni sehemu ya Mkutano wa Kimataifa unaolenga kujadili kamisheni ya hadhi ya mwanamke katika ya Wanawake Duniani (CSW69) Beijing Machi 18, 2025 Jijini New York Marekani.
Viongozi hao wamekubaliana kuangazia zaidi fursa kwa wanawake ili kuweza kuondoa ukatili wa kijinsia uliopo katika jamii zao na kuwainua wanawake kiuchumi na kiteknolojia kupitia tehama.
More Stories
PDPC yazitaka taasisi za umma,binafsi kujisajili
Abiria mil.2.1 wasafirishwa na SGR,bil.59 zakusanywa
CCM Dar yahamasisha wananchi kujiandikisha daftari la mpiga kura