Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online,Dar
SERIKALI imesema Tanzania inatarajia kunufuaika zakupitia maonesho ya Kimataifa Expo 2020 Dubai yanayoendele Katika nchi za falme ya kiharabu kwa kutangaza miradi mbalimbali iliyotekelezwa pamoja na kusaidia kupata masoko ya bidhaa za kimkakati .
Maonesho hayo ambayo yanaendelea kwa sasa nchini Dubai yamenza Oktoba Mosi ambapo yamekutanisha nchi 191 ikiwemo Tanzania ambapo zitaweza kupata fursa mbalimbali.
Hayo yamebainishwa Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara,Dotto James ,wakati akizungumza na waandishi kuhusu Maonesho hayo ambayo yanaendelea Katika nchi za falme ya kiarabu ambayo yalianza kufanyika Octoba 1 mwaka huu
Amesema ushiriki wa Tanzania Katika maonesho hayo ni kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) huku kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda.
James amesema maonesho hayo ufanyika kila baada ya miaka mitano ambapo Makampuni, Wafanyabiashara na wadau mbalimbali uonesha bidhaa zao kwa muda wa miezi sita pamoja na kupata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali
“Nchi ya Tanzania Kupitia maonesho haya imejipanga Katika kuoenesha juhudi mbalimbali zilizofanywa na serikali Katika kuanzisha na kuendeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya miundombinu ambayo itaunganisha bara la Afrika na duniani kwa ujumla”alisema
Alibainisha kuwa Kupitia maonesho hayo Tanzania itaweza kutangaza miradi ya kimkakati ikiwemo mradi wa kufufua Umeme wa Julias Nyerere (JNHPP), Reli ya kisasa(SGR), Upanuzi wa Bandari ya Dar es salaam, Ujenzi wa Viwanja vya Ndege na uimarishwaji wa usafiri wa Anga.
Amesema miradi hiyo ni kivutio na kichocheo cha ukuaji wa Biashara na uwekezaji hususani Katika sekta za Kilimo na Viwanda.
Hata hivyo amesema kuwa nchi ya Tanzania inatumia fursa hiyo kwa kushirikiana na sekta binafsi kutangaza na kutafuta masoko ya uhakiki na endelevu ya bidhaa zitokanazo na mazao ya kimkakati Kama vile kahawa, korosho, Chai, Mkonge, Karafuu, Viungo pamoja na bidhaa za ngozi .
“Zipo faida nyingi za kushiriki maonesho haya ya Expo Dubai 2020 ikiwemo Kuvutia wabia kwa ajili ya uwekezaji na kuendeleza sekta mbalimbali za kiuchumi, kutoa fursa kwa Makampuni kujitangaza na kunadi bidhaa na Huduma zinazopatikana Nchini ili kupata masoko endelevu”alisisitiza na kuongeza kuwa
“Pia vivutio vya kitalii vya kitanzania vitatagazwa pamoja na kutangaza lugha ya kiswahili, utamaduni na desturi za kitanzania”amesema
Vilevile amesema Katika maonesho hayo lipo Banda Kuu la Tanzania ambalo linahusisha Wizara, Taasisi za Serikali na Jumuiya za Wafanyabiashara
Alisema katika Maonesho hayo nchi ya Tanzania imejipanga kuonesha fursa kubwa zilizopo ikiwemo kutangaza mazao ya kimkakati ikiwemo zao la kahawa pamoja na miradi mikubwa ambayo inatekelezwa ili nchi iweze kuwa kivutio kwa wawekezaji kuja kuwekeza.
Kwa upande wake katibu mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNDC ),Dkt Godwill Wanga ambaye alikuwa miongoni ya watendaji waliokwenda kushudia maonesho hayo amesema kutokana na kutangaza Miradi mikubwa inayofanyika hapa nchini ni wazi imewapa nguvu ya Wawekezaji kuja kuwekeza hapa nchini kutokana na miradi hiyo kukukammilika.
Amesema Februari 26 hadi 27 kutafanyika kongamano la Tanzania Day ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ataweza kuhutubia katika mkutano huo.
“Kupitia kongamano hili Rais Samia Suluhu Hassan atapata fursa ya kuutubia ambapo ataweza kuzungumza pia miradi mbalimbali ya kimkamkati ambayo imefanyika nchini Tanzania”amesema.
Naye ,Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania(TPSF),Francis Nanai,ambaye aliwakilisha Sekta Binafsi katika Maonesho ya Expo 2020 Dubai,alisema Maonesho hayo yamekuja kipindi muhafaka ambapo Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan,ambaye amesema nia Serikali yake ni kufungua nchi katika uwekezaji.
Amesema maonesho hayo ni ya Kimatafa na makubwa kwani yatatoa fursa kwa nchi ya Tanzania kuona na kujifunza mambo mbalimbali hivyo alitoa wito kwa watanzania kwenda kushiriki na kujifunza vitu kutoka kwa mataifa mengine.
More Stories
Maghorofa Kariakoo mikononi mwa Tume
ITA chatakiwa kutoa mafunzo ya viwango vya juu na kasi ya maendeleo ya Kisayansi
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi