Na David John,Timesmajira Online
MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade) na Wakala wa Barabara Tanzania (TanRoads) kuboresha na kukarabati miundombinu ya ndani na nje ya viwanja vya maonesho J.K Nyerere Sabasaba wilayani Temeke.
Kikao kazi hicho kimefanyika Juni 15 2023, katika ofisi za Tan Trade jijini Dar-es-Salaam na kuhudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tan Trade Latifa M. Khamis, na wataalam kutoka Tanroads Mhandisi Haruin Rashid Senkuku, Mhandisi Elisony Edward Mweladzi, Mhandisi Raymond Godfrey Maimu pamoja na wajumbe wa mkutano huo kutoka mamlaka hiyo.
Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Tan Trade Latifa amesema wameamua kushirikiana na Tanroads katika kuboresha miundombinu ya uwanja ili kuchochea mabadiliko makubwa na kuyapa zaidi mvuto maonesho ya mwaka huu pamoja na kuleta urahisi wa kufanya biashara.
“Lengo ni kuendelea kuboresha miundombinu ya maonesho ili kuweka mazingira mazuri ya uoneshaji wa bidhaa kwa wafanyabiashara pamoja na watembeleaji na kuleta matokeo yenye tija” amesema.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu