November 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tanga kutumia vituo 5405,kupiga kura leo

Na Hadija Bagasha, Timesmajira Online,Tanga

MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi, Dkt.Batilda Burian amesema Mkoa wa Tanga una vituo 5405 vitakavyotumika kupigia kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika leo Novemba 27,mwaka huu.

Dkt Burian,ameyasema hayo Novemba 26,2024,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea uchaguzi huo ambapo,amesema maeneo yote ambayo yatatumika kwenye upigaji wa kura wameshayakagua na utayari up

Amesema,anaamini watu wa Tanga ni waastaarabu na wasiotaka fujo waende kupiga kura wakijua kwamba Mkoa huo ni ya amani na Tanzania ni ya amani.

“Tukapige kura kwa sababu muda wa kupiga kura ni mchache kuliko tuliotumia kwenye uandikishaji,na vituo vya kupiga kura vitafunguliwa asubuhi na saa 10 ndio muda wa mwisho kufika kituoni ,hivyo nawasihi wananchi tutumie fursa ya kupiga kura ili tuweze kuchangua viongozi,”.

Hata hivyo amevitaja vyama ambavyo vitashiriki kwenye uchaguzi huo kuwa ni CCM,ACT,CUF,Chadema,NCCR ,NLD,SAUTI na UDP.

“Katika Mkoa wetu huu tuna vijiji 763, vitongoji 4528, mitaa 270,Halmashauri 11 miji midogo mitatu Mombo, Lushoto na Muheza.Pia tuna Jumla ya Kata 245 na katika kipindi cha uandikishaji, hatua ya mchujo na kwenda kwenye kampeni hatujapata changamoto yoyote kutoka kwenye vyama vya siasa hiyo yote ni kuhakikisha tunakwenda kwenye uchaguzi tukiwa wamoja na kusonga mbele,”.