Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limechangia kiasi cha Shilingi Milioni Ishirini kwa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), ili kusaidia na kuwezesha matibabu ya watoto wenye vibiongo katika hospitali hiyo.
Akizungumza katika Mbio fupi za kuchangia matibabu hayo (Moi marathoni) Juni 27,2021, katika viwanja vya chuo cha udaktari Muhimbili MUHAS, Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Johary Kachwamba amesema kuwa TANESCO imeona umuhimu wa kurudisha kwa jamii sehemu ya kile inachokipata kupitia mauzo ya Umeme kwa kusaidia matibabu ya watoto hao.
“TANESCO imeamua kuangaza maisha ya jamii yetu kwa namna ya tofauti, tunafarijika kwamba matibabu haya yataokao uhai na kurejesha furaha kwa watoto wenye vibiongo,” amesema Bi. Kachwamba.
Sambamba na kuchangia kiasi hicho, wafanyakazi wa TANESCO pia wameshiriki katika kukimbia mbio hizo katika makundi ya km 5, km 10 na km 21, ambapo mshindi wa tatu mbio za km 5, kwa upande wa Wanaume ni Bw. Sebastian Kwayu, kutoka TANESCO.
Mgeni Rasmi aliyepokea hundi kwa niaba ya MOI katika tukio hilo ni, Mhe. Tulia Akson, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo alitoa shukrani kwa wote waliochangia ikiwa ni pamoja na TANESCO.
More Stories
Bei za mafuta Novemba 2024,zaendelea Kushuka
TARURA yaomba Mkandarasi aitwe
Ilemela yakusanya bilioni 3.7.robo ya kwanza