Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online, Dar es Salaam
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO), kwa kuonesha linaendelea kuwajali wateja wake, leo Julai 7,2023 katika viwanja vya maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa, maarufu kama Sabasaba yanayofanyika jijini Dar es Salaam, linatoa tokeni za umeme bure kwa wateja wake wanaotembelea banda lao katika maonesho hayo.
Akizungumzia juu ya ofa hiyo ambayo imeanza kutolewa Julia 7,2023, ambayo itafikia kikomo saa 12:00 jioni leo ambayo imetolewa kwa wananchi wote wanaotembelea banda la TANESCO na kujibu maswali ya ufahamu wanayoulizwa na watoa huduma wa Shirika hilo.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji Umeme Tanzania, Athanas Sinangali, amesema katika banda lao wamejipanga kikamilifu kwa ajili ya kutoa huduma kwa wateja wake wote, ikiwa pamoja na kujibu maswali ambayo wateja wake wanahitaji kufahamu na mradi wa bwawa la Nyerere.
“Kwa kutambua mchango wa wateja wetu, hivyo leo tumeona ni vyema tukarudisha kwa jamii kwa kutoa unite za umeme bure kwa wateja wetu wote wanaotembelea banda letu…akifika hapa kuna swali la ufahamu ataulizwa na akijibu vizuri atapata unite kuanzia 50 na akijibu vizuri zaidi basi atapata unite zaidi ya hizo bure” anasema Sinangali.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuweza kutumia vyema maonesho hayo kwa kuhakikisha wanafika katika banda la TANESCO, ili waweze kujionea kazi zinazofanywa na shirika hilo ikiwa ni pamoja na kujifunza vitu mbalimbali vinavyohusu masuala ya nishati ya umeme.
More Stories
Polisi yaonya vyama vya siasa
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia
Kujenga ofisi ya kisasa,akipewa ridhaa ya Uenyekiti