June 6, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TANESCO yashinda tuzo ya uhifadhi mazingira kupitia mradi wa JNHPP

Na Penina Malundo, Timesmajira

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limekabidhiwa tuzo ya uhifadhi wa mazingira katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Kitaifa yaliyofanyika jijini Dodoma leo tarehe 05 Juni, 2025.

Tuzo hiyo imetolewa kutambua mchango wa TANESCO katika kuhifadhi mazingira kupitia utekelezaji wa Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), ambao umeendelea kuzingatia misingi ya utunzaji wa mazingira sambamba na kuchangia kupunguza gesi joto.

Tuzo hiyo ilitolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, na kupokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Lazaro Twange, katika hafla ya kufunga rasmi maadhimisho hayo.

Kupitia ushiriki wake katika maonesho hayo, TANESCO imeendelea kuonesha dhamira ya dhati ya kutekeleza miradi mikubwa ya umeme kwa kuzingatia usalama wa mazingira, ikiwa ni pamoja na JNHPP na mingine inayolenga kuleta manufaa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.