December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tanasha: Mimi sio mwanamke wa kuamka asubuhi na kupika

MSANII wa muziki na aliyekuwa mzazi mwenzie msanii wa Bongo fleva na Bosi wa Wasafi Diamond Platnumz, Tanasha Dona amesema, yeye sio mwanamke wa kukaa nyumbani na kuamka asubuhi kupika kutokana na utamaduni aliouzoea.

Tanasha raia wa Kenya Tamaduni aliyoizoea yeye ipo tofauti na ile aliyoikuta kwa aliyekuwa mpenzi wake Diamond kwani mila na desturi zilikuwa tofauti jambo ambalo familia yake ilichangia penzi lao kuvunjika.

“Nilikuwa nikitoa pesa zangu zote, Wakati mwingine nilikuwa nikihukumiwa kwa sababu mimi sio mwanamke wa kitamaduni ya Kitanzania. Sijakaa nyumbani, kuamka na kupika. Ninapenda kupika lakini ikiwa naweza kuajiri mpishi kwanini nisifanye hivyo,? Nilikumbana na vizuizi vingi, Watu wengi pamoja na familia hawakutaka niwe Diamond,” alisema Tanasha.

Hata hivyo, mwanadada huyo raia wa Kenya mwenye asili ya Italia, mwenye Shahada ya Chuo Kikuu aliyoipata nchini Ubelgiji yupo tofauti na tamaduni za Kiafrika jambo ambalo lilikuwa likimsumbua sana Tanzania.