January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TanaPlay kuleta mapinduzi ya muziki Tanzania

-Ni Aibu kwa Muimbaji Wa Muziki wa injili kuwa masikini

Na Queen Lema, TimesMajira Online, Dar es saalam

Waimbaji wa Muziki wa injili hapa nchini wametakiwa kuzingatia ubora wa kazi zao, ili kuleta ushindani katika tasnia hiyo ya Muziki ndani na nje ya nchi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa kampuni ya Muziki hapa nchi TanaPlay Mudic Platform Bwana Daniel Mngoma Dcom, wakati akizungumza na Gazeti hili, ofisini kwake Ukonga, Dar es salaam.

Mkurugenzi huyo amebainisha kwamba, sanaa ya Muziki pamoja na huduma kwa Ujumla imekua ikipata changamoto hasa sokoni, kutokana na ubora wa kazi kuwa chini.

“Ninapozungumzia ubora namaanisha kuanzia Audio na kisha Video, Sisi kama TanaPlay tumekuja na suluhisho ambalo naamini Muziki wetu wa injili utakuja kuheshimika zaidi na hatimae waimbaji watajivunia kuitwa katika wito huo” Amesema Dcom

Mbali na hayo ameeleza kuwa, TanaPlay imeanzisha studio za kurekodi Muziki hapa nchini ikiwa ni sehemu ya kuleta mapinduzi katika Muziki wa injili pamoja na kuwaheshimisha waimbaji.

“Waimbaji wetu wengi ni masikini, na wengi wanategemea kuimba ibadani wapewe nauli ndio warndeleze maisha yao, matokeo yake wanadharaulika na wengine wanakata tamaa kabisa, sasa hii sio hali nzuri kwa watu waliopewa zawadi kubwa ya sauti na Mungu, sasa hii tumekuja kuibadilisha”.

Ameongeza DcomTanaPlay ni kampuni ya Muziki hapa nchini ambayo imefingua dtudio zake hivi karibu za kurekodi audio pamoja na video, Huku wakitegemea kuzindua kampeni maalumu ya Mapinduzi ya Muziki wa Injili Hivi karibuni.