December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TANAPA yatoa elimu kwa wananchi kuhusu Uhifadhi, Uwekezaji, Utalii

Na Hamisi Miraji, Timesmajira Online

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), limesema katika msimu huu wa Maonesho ya 48 ya Biashara maarufu kama ‘Sabasaba’ wapo kwa ajili ya kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu maana ya Uhifadhi, Uwekezaji na Utalii.

Akizungumza na gazeti la majira Julai 6, mwaka huu, Mhifadhi kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Eunice Msangi amesema Shirika hilo limeshiriki maonesho hayo wakiwa na malengo makubwa matatu.

Amesema, lengo la kwanza ni kuelemisha jamii kuhusiana na Uhifadhi, la pili kuelimisha jamii kuhusu kundi la Uwekezaji kutoka katika hifadhi za Taifa na tatu ni utalii, kwa maana wapo hapo kwa ajili ya kutangaza vivutio vy utalii vilivyomo katika hifadhi zetu.

Eunice, amesema kupitia maonesho hayo ya 48, TANAPA wanaamini wananchi watajifunza mambo mbalimbali yanayohusiana na Hifadhi za Taifa, lakini pia Dunia itaelewa kuwa Tanzania ni mahali sahihi pa kuwekeza. lengo likiwa wananchi waelewe dhamila ya uwekezaji ili wajitokeze kuwekeza.

“Unapotangaza Utali, utalii nao unaongezeka kwa sababu kunahitajika huduma nzuri kwa hao watalii na hasa huduma za maradhi, kwa hiyo tunaamini wananchi wanapojitokeza tunapata kuwekeza kwenye Hifadhi za taifa tunaongeza idadi ya watalii wengi.

“Lakini pia tunahamasisha wananchi wazielewe hifadhi zao, Tanzania kuna hifadhi ya Taifa ipo kusini mwa nchi yetu, Hifadhi ya Nyerere na Ruaha, hifadhi hizi mbili ni kubwa kwa hiyo tunahamasisha pia watu wawekeze kwenye hayo maeneo ili taifa liwe na muktadha huo,” amesema Eunice.

Hata hivyo amesema, sababu kubwa ya kuhamasisha wananchi walewe mbuga hizo wengi wao wamekuwa wakitembelea mbuga za Kilimanjaro, Serengeti, hivyo watanzania wanatakiwa watambue Kusimi mwa Tanzania napo kuna fulsa kubwa sana.

Pia amesema, wameandaa vipeperushi vya kuhamasisha wananchi watembelee hifadhi za taifa ikiwemo hifadhi ya taifa ya Nyerere, Mikumi, Tarangire, Odzungwa na Mkomanzi. Hivyo kwa wale mbao wapo tayari watembelee banda la shirika hilo kwa ajili ya kujiandikisha.

Mbali na kutoa elimu hiyo lakini pia katika msimu huu TANAPA, inahamasisha watanzania kupigia kura hifadhi ambazo zinawania Tuzo za za World Travel Award 2024.

Hufadhi ambazo zinatakiwa kupigiwa kura ni Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Kilimanjaro ambazo zinawania tuzo za World Travel Awards katika kipengele cha Africa’s leading national park wakati Kilimanjaro ikiwania tuzo katika kipengele cha Africa’s leading tourist attraction.

Hifadhi ya Taifa Serengeti ambayo imeshinda tuzo ya kuwa hifadhi bora Afrika mara tano (5) mfululizo hivyo inawania ya sita ili iweze kupaa juu zaidi.

“TANAPA tumahamasisha zoezi ili hifadhi zetu zishinde na zikishinda tunazidi kujitangaza zaidi duniani, lakini pia uongezeko la utalii utakuwa mkubwa na taifa litaingiza kipato,” amese Eunice.

Hata hivyo amesema, kutokana na kuwahamasisha kupitia kampei ya ‘VOT NOW’ hamasa imekuwa kubwa hasa kupitia maonesha hayo, watu wengi wamejitokeza ili kutaka kujua namna ya kupigia kura hifadhi zao.

Amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye banda la TANAPA, ili kupata elimu kuhusu mambo mbalimbali yanayofanywa na shirika hilo.