December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TANAPA yashiriki mkutano wa sita wa Utalii Namibia

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA), Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) pamoja na wadau mbalimbali kutoka Tanzania wanashiriki Mkutano wa sita wa vijana katika Utalii ulioanza jana tarehe 28/05/2024 jijini Windhoek, Namibia.

Mkutano huo umehudhuriwa na vijana zaidi ya 30 kutoka mataifa mbalimbali Duniani, ambapo kwa siku ya kwanza umegusia masuala muhimu ya Utalii, Ujasiriamali na Uwekezaji ambayo yametolewa na washiriki kutoka Mataifa mbalimbali.

Hata hivyo mkutano huo utakaofanyika kwa siku nne kuanzia Mei 28 hadi 31 Mei, 2024, umejikita kuwanoa vijana hao katika masuala ya utalii na uwekezaji ili wawe msingi imara katika kukuza sekta ya Utalii barani Afrika na Dunia kwa ujumla.