Na Penina Malundo,Timesmajira
CHAMA cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA),kimelaani vikali aina yoyote ya mashambulizi ya kijinsia dhidi ya wanawake, hasa viongozi wa kisiasa, kupitia mitandao ya kijamii.
Akizungumza hayo leo Juni 27,2025,Mwasisi wa Chama hicho, Halima Sharif wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho ambao umehudhuriwa na wanachama wake amesema Tamwa inaamini kuwa mwanamke mwanasiasa anapaswa kuhukumiwa kwa hoja na misimamo yake ya kisera, siyo kwa sababu ya jinsia yake.
Amesema kuudhalilisha wanawake wa kutumia majukwaa ya kidijitali ni ukiukwaji wa maadili ya Kitanzania na kikwazo kwa maendeleo ya demokrasia jumuishi. “Pamoja na changamoto hizi, TAMWA inaendelea kujivunia mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais wa kwanza
mwanamke wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan hasa katika uteuzi wa wanawake wenye uwezo mkubwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika taasisi na medani za siasa,”amesemaÂ

Amesema ili kujenga imani zaidi wanawake walio katika nafasi za uongozi wanapaswa kujifunza kwa Rais Samia, wakitambua kwamba katika jamii ya watanzania hii siyo tu ni viongozi bali pia wanatumika kama kioo cha kupima uwezo wa mwanamke katika uongozi.
” Kufanya kwao vyema kama tunavyoona kwa Rais wetu, itawaongezea ari na kujiamini wanawake na wasichana kuzushi ndoto zao za kuwa viongozi,Uongozi wa Rais Samia umeonesha kwa vitendo kuwa wanawake wanaweza kuongoza kwa mafanikio kama ilivyo kwa wanaume.
” Kupitia dhamira yake ya kuendeleza taifa, tumeona utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo, marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa, na mchakato wa maboresho ya sheria ya uchaguzi ukipiga hatua,”amesisitiza.
Amesema TAMWA inaendelea kusimamia misingi ya usawa wa kijinsia, kuwaunga mkono wanawake walioko katika uongozi na kuandaa mazingira salama na jumuishi kwa wanawake wote kushiriki kikamilifu katika siasa huku tukikemea vikali aina zote za udhalilishaji, mitandaoni na nje ya mitandao.

Betty Mkwasa ambaye ni Mwanachama mkongwe wa TAMWA, ameelezea nafasi ya TAMWA katika Uongozi wake, amesema kuwa amekuwa kiongozi katika uandishi wa habari na katika serikali kuwa Mkuu wa Wilaya ya Koroge Tanga.
Amesema kuwa TAMWA imempa ujasiri wa kupambana na unyanyasaji wa kijinsia kwa Wasichana na Wanawake akitolea mfano Tanga alikuta wasichana walikuwa hawahudhurii shuleni na matokeo ya wanafunzi kuwa hafifu sana.
“Kwa mafunzo ambayo niliyapata TAMWA na harakati ambazo nilijifunza nikiwa TAMWA niliweza kufanya kampeni ambazo zilihakikisha watoto wote ambao wanatakiwa kuwepo shuleni wanarudi shule, nilifanya kampeni hiyo kwa kuwashirikisha wazazi na viongozi wote kuanzia ngazi za vijiji mpaka wilaya.
“Tulifanya kampeni ile na kuwafata watoto popote pale walipo wakifanya shughuli mbalimbali na kuwarudisha shuleni.” Ameeleza
Amesema kuwa aliweza kuwarudisha watoto kama 400 hivi shuleni ambao walikuwa wameshaondoka na kwenda kufanya shughuli mbalimbali.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako