Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.
SERIKALI kupitia Ofisi ya Rais,TAMISEMI imewaagiza wakurugenzi wa halmashauri wote nchini kuweka utaratibu maalum wa kuwatambua na kuwabaini wafanyabiashara wanaouza bidhaa katika maeneo ya shule ili kusaidia kukabiliana na changamoto ya matumizi ya dawa za kulevya.
Kauli hiyo imetolewa jijini hapa leo, Novemba 30,2022 na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Ramadhan Kailima wakati akifungua kongamano la 14 la wanataaluma katika Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI),Hombolo ikiwa ni maandalizi kuelekea Mahafali ya 14 ya Chuo hicho yatakayofanyika kesho chuo hapo ambapo wanahitimu wanachuo 4923.
Amewataka wakurugenzi wote nchi nzima kwa kushirikiana na kamati za shule waangalie na watafakari namna ya kuwatambua na kuwabainisha wafanyabiashara wote wenye vitendo hivyo.
“Wanauza pipi na zile biskuti nitumie fursa hii kuwaasa wakurugenzi wa halmashauri wote kwamba wale wanaoenda kuuza pipi kwenye maeneo ya shule zetu watafute namna ya kuwatambua hao watu kwa kujua uhakika wao hao wauzaji tunawajua wanatoka wapi mitaa na vijiji wanavyotoka tuwajua ili isaidie kufukuza janga hilo,
“Ni hatari kwasababu akianza kutafuna ile pipi kwa mara ya kwanza atajisikia vizuri baada ya muda anajisikia kuumwa kwasababu ya pipi ya mia moja,mia mbili,”aamesema Kailima.
Kailima alitoa maagizo hayo kwa Wakurugenzi kutokana Novemba 15,2022 Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Dawa za kulevya, Gerald Kusaya kuwaambia waandishi wa habari kwamba kuna wimbi kubwa la uwepo wa vyakula ambavyo vingi, ni vile vinavyopendwa na watoto kutengenezwa na dawa za kulevya,hivyo amewaomba Watanzania hasa wazazi kuwa makini na watoto wao.
Aidha Naibu Katibu Mkuu huyo amekiagiza Chuo cha Serikali za Mitaa (HOMBOLO),kufanya utafiti ili kubaini sababu za baadhi ya hoja za halmashauri kujirudia katika ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG).
Pamoja na kurudisha utaratibu wa kutoa mafunzo kwa madiwani pindi wanapochaguliwa ili kuondoa migogoro baina ya viongozi wa serikali za mitaa.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo hicho,Dkt.Mashala Lameck amesema lengo la kongamano hilo kuwa nikujadili mada za wanataaluma ambapo ametaja mada ya mwaka huu kuwa ni mchango wa mamlaka za Serikali za mitaa katika kufikia dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka 2025.
“Tutawasilisha mada na wanataaluma watachangia na sisi kama chuo tunaowajibu sasa kufikia dhira hiyo kupitia shughuli zetu tunazozifanya sisi ambazo ni mafunzo kupitia huduma za ushauri lakini tunafanya haya yote katika Serikali za mitaa tukiamini sisi tunawajibu na tumepewa jukumu na Serikali la kuwa chuo kiongozi cha mafunzo yanayoendeshwa katika Serikali za mitaa.
Naye Naibu Mkuu wa chuo utafiti na ushauri Dkt.Michael Msendekwa amesema kuwa wamepokea maagizo waliyopewa kuhusu madawa ya kulevya,kuwa mafunzo viongozi wa serikali za mitaa pamoja na kufanya utafiti wa hoja za Mkaguzi mkuu wa serikali na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI na watayafanyia kazi.
“Tumelipokea hilo tutaendelea kulifanyia kwa weledi tunayo huwa tunafanya kwasababu ni msisitizo tutaendelea sasa lakini ameongea mengi kuna watumishi pia hawa watendaji wa vijiji,kata na mitaa lakini kwenye vitongoji pia kuna wenye viti pia hawa wawezekupatiwa mafunzo mara kwa mara na chuo cha serikali za mitaa,”amesema Dkt.Msendekwa.
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja