Na Rose Itono,Timesmajira
CHAMA Cha Usambazaji wa Sekta ya Madini Tanzania (TAMISA) kimeandaa Kongamano Maalumu la kuwajengea
uwezo Watanzania kushiriki kwenye shughuli za Uwekezaji katika sekta ya madini
Akizungumza na Waandishi wa Habari Dar es Salaam leo Mwenyekiti wa TAMISA Peter Kumalilwa amesema
wanatarajia Waziri wa Madini Antony Mavunde kuwa mgeni rasmi kwenye Kongamano hilo ambapo litafanyika Mei 16 mwaka huu
” Mei 16 mwaka huu TAMISA tunatarajia Waziri Antony Mavunde atazindua Kongamano Maalumu la kuwajengea uwezo Watanzania kushiriki katika Uwekezaji wa Sekta ya.madini,” alisema Kumalilwa na kuongeza kuwataka Wazawa wa kitanzania kuacha kubaki nyumba kwa kujiunga na TAMISA ili kuzifahamu fursa zinazopatikana kwenye Uwekezaji wa sekta hiyo
Ameongeza kuwa, uzinduzi huo pia utaenda sambamba na uzinduzi wa Kamati Maalumu ya kutoa taarifa mbalimbali kuhusu uwekezaji kwenye sekta hiyo

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati TAMISA Dkt. Sebastian Ndege alimpongrza Rais wa Jamhuri ya Muu gano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufungua Uwekezaji wa sekta hiyo kwa wajasiriamali wa kitanzania kwa kusema kuwa kuwa fursa hizo zitawawezesha wengi kunufaika kiuchumi
Amesema TAMISA imejipanga kuwa na makongamano ya mara kwa mara ili kuweza kuwaweka pamoja Wadau wa sekta hiyo ealiopo nchini na kukumbushana fursa zilizopo
‘ Mpaka sasa TAMISA Ina wanachama zaidi ya 50 ambapo wamekidhi vigexo kwa kuzingatia ukubea wa Uwekezaji huo na tunawaomba Wadau wengine wa sekta hiyo kuona umuhimu wa kujiunga ili kubadlishana uxoefu na kutambuana zaidi,” amesema
Amesema kuwepo kwa makongamano ya mara kwa mara yanayoandaliwa na TAMISA kutatoa fursa ya kuwaweka pamoja Wadau wa sekta hiyo
“Tunawasihi watanzania wenye makampuni yanayotoa huduma katika sekta hiyo kujiunga na TAMISA ili kupata taarifa mbalimbali zinazohusu sekta hiyo,” amesema Dkt Ndege
Aidha ametaja lengo la kuanzishwa kwa TAMISA kuwa ni pamoja na kuboresha maudhui ya ndani, kuimarisha mazingira ya biashara kukuza utamaduni wa uvumbuzina ushirikiano Kati ya wadau na uendelevu wa biashara ndani ya mfumo wa maudhui.
More Stories
WMA yahakiki vipimo asilimia 99 ya lengo
Rais Mwinyi:Tutamuenzi Charles Hilary kwa utendaji wake uliotukuka
Kapinga :Serikali inaendelea kutekeleza miradi ya umeme kwenye maeneo ya kimkakati