Judith Ferdinand,Timesmajira Online,Mwanza
Tamasha la Chifu Hangaya Utamaduni 2025(Chief Hangaya Utamaduni Festival 2025),kufanyika Machi 8,2025,ili kutoa fursa kwa jamii ikiwemo watoto kujifunza na kujikumbusha tamaduni za makabila mbalimbali nchini Tanzani sanjari na kukuza sekta ya utalii.
Akizungumza na waandishi wa habari uliofanyika Machi 5,2025,Mkurugenzi wa Cheza Kidansi Entertainment ambao ndi waandaaji wa tamasha hilo,Bernard James,amesema,tamasha hilo litafanyika Machi 8,2025,siku ya mwanamke duniani, uwanja wa Furahisha uliopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza,lengo ni kuwapongeza wanawake nchini Tanzania akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan,ambaye ni mkuu wa machifu na mwanamke namba moja ,ambaye anamchango katika kuenzi tamaduni za kitanzania na kukuza utalii.
“Huwezi kutofautisha utamaduni na utalii,kwani watu wengi wanakuja nchini hapa kujifunza lugha ya Kiswahili ambayo ni sehemu ya utamaduni na wanavutiwa nazo tamaduni zetu,hivyo tunaingiza fedha za kigeni,kuajiri watu wengi.Tukaona ni lazima tuwapongeze wanawake wote nchini akiwemo Rais Samia,na kuhakikisha utamaduni wetu unatengeneza fursa zaidi,”.
Bernard,anasema,tamasha hilo halina kiingilio na watu watashiriki bure,hivyo amewahamasisha wananchi wa Mwanza kujitokeza kwa wingi siku hiyo kwani watapata fursa ya kushuhudia na kujifunza tamaduni za makabila mbalimbali ikiwemo vyakula,mavazi na vingine vingi.
“Tamasha hilo litatoa fursa ya watu kushiriki mbio za kilomita 5 kuanzia uwanja wa Furahisha hadi Mjini kati na kurejea Furahisha,pia kutakuwa na maonesho ya biashara na bidhaa mbalimbali za asili kutoka kwa wajasiriamali nchini,maonesho ya mavazi ya asili,utani wa makabila na sababu za msingi za kutaniana,michezo ya asili,burudani za muziki na ngoma za makabila,vyakula na vinywaji vya asili,”.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara(CBE),Kampasi ya Mwanza,Dkt.Robert Mashenene,amesema,watashiriki katika tamasha hilo kwa kutoa elimu ya ujasiriamali bure kwa wananchi ikiwemo utunzaji kumbukumbu,fedha,dijitali.,ambapo kwa mwaka jana chuo hicho kilitoa elimu kwa wajasiriamali 1500 nchini bure huku kwa Jiji la Mwanza walikuwa 250.
Mjumbe wa Bodi ya Hospitali ya St.Clare Pius Kamala,anasema,watashiriki katika tamasha hilo kwa ajili ya kuhamasisha jamii kufanya suala la kupima afya kuwa ni utamaduni.”Watanzani wengi kupima afya siyo utamaduni wetu bali ni kitu ambacho kinatokea kama ajali,mara nyingi tunasubili mtu uugue alafu aende hospitali,na wakati mwingine tunapelekwa kwa kutotaka tukiwa tumeisha zimia.Hivyo tumefurahi kuwa tumepata jukwaa ambalo tutatumia kuwaeleza watanzania kuwa afya inadidi iwe sehemu ya utamaduni wetu,”.
Meneja wa kampuni ya mtandao wa simu YAS,Robert Sanyagi,anasema,kupitia tamasha hilo litarithisha utamaduni wa kitanzani kwa watoto na litafungua fursa ya kibiashara na kampuni hiyo itatumia tamasha hilo kueleza wateja wao maboresho waliofanya ya kiteknolojia.
Hata hivyo,Mwakilishi wa kampuni ya usafirishaji ya Jorafra Transport Agency Sales and Markerting,Loveness Gustaph,anasema katika tamasha hilo watarejesha kwa jamii na kusherekea siku ya mwanamke duniani kwa kutoa vifaa vya kujistiri watoto wa kike.
More Stories
Wanawake wametakiwa kuhakikisha wanampa kura za heshima
Maadhimisho miaka 30 ya VETA kufanyika Dar
Wananchi waaswa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha Daftari la Mpiga Kura