Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online, Dar es Salaam
TAMASHA la Oktobafest lililoandaliwa na Kampuni ya Serengeti Breweries Limited, ambalo lilifanyika jana kwenye viwanja vya Coco Beach jijini Dar es Salaam, limekonga nyoyo za mashabiki hapa nchini, kutokana na wasanii kuonesha uwezo mkubwa jukwaani.
Tamasha hilo ambalo lilikuwa la kipekee limejizatiti kutoa burudani ya kiutamaduni zaidi, kusherehekea utamaduni wa Tanzania kupitia bia, muziki, mitindo, na chakula.
Kupitia Kampeni ya Inawezekana, Kampuni ya Serengeti Breweries Limited imejitolea kuhamasisha unywaji wa kistaarabu, kuhakikisha kwamba washiriki wanafurahia tamasha kwa kistaarabu na hawaweki hatarini usalama wao.
Akizungumzia Tamasha hilo, Meneja wa Mawasiliano na Uendelevu wa Serengeti Breweries Limited, Rispa Hatibu amesema Oktobafest ni Tamasha la kwanza kubwa kufanyika hapa nchini, kupitia Bia ya Serengeti Lite.
“Tamasha hili ni lakwanza kubwa kufanyika nchini Tanzania, ambalo halijawahi kutokea kuandaliwa na Kampuni ya Serengeti Breweries Limited, likiwa na lengo la kuonesha Tamaduni mbalimbali za Kitanzania.
“Tamasha hili linafanyika nchi tatu za Afrika Mashariki, ambalo limeanza na Tanzania Oktoba 21, lakini Uganda na Kenya litafanyika wiki ijayo,” amesema Rispa Hatibu .
Hata hivyo amesema, wasanii waliotumbuiza kutoka nchini Tanzania ni, G nako, Ali Kiba, Chino kidd na Billnass, msanii kutoka Kenya, akiwa Nyamari Ongegu maarufu ‘Nyashinski’ huku Jose Chameleone akitokea Uganda.
Oktobafest, ni tamasha, linalenga kuunganisha mambo mbalimbali yaliyomo kwenye utamaduni wa Tanzania. Kupitia Kampeni ya Inawezekana ya Serengeti Breweries Limited.
Pia, Tamasha hilo linahamasisha unywaji wa pombe kiustaarabu ambapo washiriki waliweza kufurahia tamasha hilo la kitamaduni bila wasiwasi wowote.
More Stories
GETHSEMANE GROUP KINONDONI yaja na wimbo wa siku yetu kwaajili ya harusi
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA