Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Tamasha kubwa la Urafiki linatarajiwa kufanyika kuanzia Juni 23 hadi Juni 26 mwaka huu katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.
Akizungumza na Waandishi wa habari Muhubiri wa Kimataifa kutoka nchini Canada Mwinjilisti Dakta PETER YOUNGREN baada ya kuwasili nchini kwa ajili ya kuongoza tamasha hilo, amesema lengo la tamasha hilo ni kuwaunganisha wakazi wa Dar es salaam bila kujali itikadi za kiimani huku akisisitiza kuwa katika siku hizo watu wataponywa na kutakuwa na mabadiliko makubwa ya umoja na mshikamano miongoni mwao.
Askofu wa Kanisa la Efatha JOSEPHATH MWINGIRA amesema ujio wa Mwinjilisti YOUNGREN ni baraka kubwa kwa Watanzania kutokana na uwezo wake na karama aliyopewa na Mungu ya kuwaunganisha watu wa imani zote.
Mratibu wa Tamasha hilo Askofu wa Kanisa la CECT CHARLES SEKELWA amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi ili kufundishwa neno sahihi la Mungu ambalo litawaunganisha pamoja na hivyo kufanikisha mipango mbalimbali ya Taifa.
Kabla ya kuanza kwa Tamasha hilo Muhubiri huyo atatoa mafunzo kwa viongozi mbalimbali wa dini zote zilizopo nchini yatakayofanyika leo na kesho.
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Gridi za Tanzania, Kenya kuimarisha upatikanaji wa umeme
Mama Zainab:Watoto yatima ni jukumu la jamii yote