Na Nasra Bakari, TimesMajira Online
CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania(TALGWU),wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa ahadi alizozitoa katika maadhimisho ya Mei mosi 2022 jijini Dodoma ambazo zimejenga ari ya kufanya kazi na kuleta matumaini mapya kwa wafanyakazi ambayo yalikuwa yamepotea kwa miaka mingi.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Mkuu wa Chama hicho Rashid Mtima alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya TUCTA jijini Dar es Salaam alisema, ni furaha kubwa kuona Mkuu wa nchi anatambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na wafanyakazi wa chama hichi katika kuleta maendeleo ya Taifa.
Mtima alisema, tunamshukuru Rais Samia kwa kutuhakikishia nyongeza ya mishahara ambapo ni muda mrefu sasa watumishi wa umma hawajapandishiwa mishahara, hiki kilikuwa ni kilio chetu cha muda mrefu ambapo sasa jambo hili limeenda kutekelezwa.
“Vilevile nimshukuru Rais Samia kwa kuisikiliza kilio chetu cha muda mrefu kuhusu watumishi waliondolewa kazini kwa vyeti vya kughushi(feki).Kama chama kwa kupitia TUCTA kwa muda mrefu tulikuwa tukiomb serikali kuliangalia kundi hili la watanzania ambapo walitumikia kwa uadilifu nchi yetu lakini kwa bahati mbaya wakakubwa na kadhia hii.
“Pia tunamshukuru Rais Samia kwa kuonesha upendo mkubwa kwa watanzania ambapo walitumikia nchi yetu kwa nguvu zao zote hatimaye ameagiza wizara ya fedha na mipango kushughulikia na kuwalipa zao zinazotokana na makato ya mishahara yao.
Alisema, tunamshukuru Rais Samia kwa kuagiza mifuko ya hifadhi ya jamii na maafisa utumishi kuhakikisha wanashughulikia haki stahiki za watumishi wanaotarajiwa kustaafu ndani ya miezi sita ili pindi inapofika mtumishi anastaafu mafao yake yawe yatari, tunamshukuru sana kwa agizo hili kwani wanachama wetu wamekuwa wakitaabika sana baada ya kustaafu kwani wengi wao hutegemea mafao hayo kwa ajili ya kuendeleza maisha yao.
“Pia tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Rais Samia kwa kuudwa kwa bodi ya kima cha chini cha mishahara kwa sekta ya umma ambayo amesema imeshaanza kufanya tathimini ya mishahara iiliyopo sasa na kuagiza wizara zinazohusika kuiwezesha bodi hiyo ili kutekeleza majukumu yake ipasavyo jambo hili lilikuwa ni kili cha muda mrefu lakini sasa limetekelezwa.
“Aidha tunamshukuru Rais Samia kwa kukemea kitendo cha baadhi ya wafanyabiashara kutafuta visingizio na kupandisha kiholela bei zaa bidhaa na kusababisha ugumu wa maisha, sote tunajua hali ya maisha ni ngumu sana lakini kitendo cha wafanyabishra kuendelea kutukandamiza kwa kuongeza bei ambako kunapunguza uwezo wa mfanyabishara kuweza kununua bidhaa na kukidhi mhitaji yake hivyo tunamshukuru Rais Samia kwa kukemea vitendo hivi,” alisema na kuongeza
Nimalizie kwa kusema kwa niaba ya wanachama wote wa TALGWU nchini napenda kutoa shukrani za dhati kwa serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia kwa kuzingatia na kusikiliza mahitaji ya muda mrefu ya chama chetu na hatimaye kutoa kauli ya kupata ufumbuzi wa changamoto hizo.
More Stories
Serikali yahimiza wananchi kutembelea vivutio vya utalii
Magunia ya kufungia tumbaku yakamatwa
Madereva 16,Mwanza wafungiwa leseni ya udereva