January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TAKUKURU yazidi kukunjua makucha

Na Mwandishi Wetu

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Temeke, jijini Dar es Salaam inamshikilia Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira Mtaa wa Tambukareli Kata ya Azimio,  Ally Mtiga kwa kujifanya ni Ofisa wa Ardhi kuomba rushwa sh.200.000  kutoka kwa mwananchi (jina linahifadhiwa).

Taarifa ya TAKUKURU kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana imeeleza kwamba mwenyekiti huyo akijifanya ofisa ardhi alitaka apewe sh. 200,000 ili aweze kumsaidia kupata leseni ya makazi ya jengo lake.

“Uchunguzi wa TAKUKURU ulibaini kwamba, Januari 26, mwaka jana, Mtiga  anayejifanya ofisa ardhi, akiwa ofisini kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa ma Tambukareli alipokea fedha hizo za mtego kiasi cha sh. 200,000 ili aweze kumsaidia mwananchi mmoja (jina limehifadhiwa) kupata leseni ya makazi ya jengo lake.

Taarifa hiyo imeeleza kwamba udanganyifu ni kinyume na kifungu cha 302 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu Sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marebisho mwaka 2002.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo TAKUKURU ilipokea malalamiko yanayomhusu Mtiga Januari 19, mwaka jana.

Taarifa hiyo imeeleza kwamba uchunguzi wa tuhuma hizo umekamilika na mtuhumiwa kufikishwa mahakamani jana na kufunguliwa mashtaka kwa kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kinyume na kifungu cha 302 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu Sura namba 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002. Mtuhumiwa huyo amesemaomewa mashtaka yake katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke.ameongeza