Zena Mohamed,Timesmajiraonline, Dodoma
KATIKA kipindi cha Miezi mitatu kuanzia Januari 1 hadi Machi 31 mwaka huu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU), Mkoa wa Dodoma imepokea jumla ya malalamiko 138 ambapo kati ya malalamiko hayo ,malalamiko 81 yalikuwa ya rushwa na walalamikaji walielimishwa na kupewa ushauri wengine saba taarifa zake zimehamishiwa idara nyingine kwa hatua zaidi.
Hayo yamesemwa jijini hapa leo ,Mei 26 ,2023 na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma,John Joseph wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taarifa ya miezi mitatu za kazi za Taasisi hiyo ambapo amesema kati ya malalamiko hayo,malalamiko 57 yalihusu rushwa ambayo yalipelekwa kufunguliwa majalada ya uchunguzi.
Joseph amesema kuwa kati ya majalada hayo 57 uchunguzi wa majalada 17 umekamilika,mashauri mawili yamefunguliwa mahakamani na majalada 15 hatua mbalimbali za kisheria zinatarajiwa kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa huku majalada 40 uchunguzi wake bado unaendelea na uko katika hatua mbalimbali za kiuchunguzi.
Ametaja idara zinazolalamikiwa kutokana na taarifa 57 ni huku elimu ikiongoza kwa malalamiko 11,TAMISEMI malalamiko tisa,sekta binafsi tisa ,Ardhi saba ,Afya saba ,polisi tano,kilimo tatu,manunuzi mawawili ,mahakama moja,maji moja,mazingira moja na fedha moja.
“Mashauri mapya manne yametolewa maamuzi ambapo hadi sasa mashauri mawili tumeshinda na mashauri tumeshindwa na jumla ya mashauri 31 yanaendelea kusiilizwa mkoani hapa na yako katika hatua mbalimbali,”amesema.
Vilevile amesema kuwa wamefanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo 36 katika mkoa wote yenye zaidi ya shilingi bilioni 16.8.
Ametaja miradi ya maendeleo iliyofuatiliwa kuwa ni elimu miradi 22,Kilimo miradi mitano,fedha mitatu,Afya minne,ardhi mmoja na ujenzi mmoja ambapo kiasi cha shilingi 1,050,000 katika Wilaya ya chamwino ziliokolewa.
Aidha amesema kuwa miradi 21 imetolewa ushauri na elimu pia ufuatiliaji unaendelea, miradi saba imekamilika,miradi miwili imetolewa maelekezo,chambuzi za mfumo ba warsha miradi miwili ,miradi miwili inaendelea na mmoja ufuatiliaji wa nyaraka ,mradi mmoja fedha ziliokolewa katika Wilaya ya Chamwino huku mradi mmoja katika Wilaya Kongwa unaendelea na uchunguzi ili kubaini upotevu wa fedha.
Sambamba na hayo amesema wameweza kudhibiti jumla ya Shilingi milioni 41.2 ambazo zilikuwa kayika hatari ya kufanyiwa ubadhirifu katika fedha za mpango wa maenedeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko 19.
Pamoja na hayo ametaja vipaumbele kwa kipindi kinachofuata cha mwezi Aprili hadi Juni mwaka huu ambapo amesema wataongeza kasi ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuziba mianya ya rushwa na ufujaji.
Pia Kuongeza kasi ya uelelimishaji umma kwa kutumia njia mbalimbali,kuongeza kasi katika kufanya chambuzi za mfumo hasa katika maeneo yanayolalamikiwa zaidi na kuendelea kuelimisha jamii na hususani kundi la vijana kupitia ushirikiano uliopo kati ya TAKUKURU na SKAUT-TAKUSKA na jamii nzima ya wana Dodoma.
Hata hivyo ametumia fursa hiyo kuwasihi Wakurugenzi wa halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma pamoja na Madiwani wote kufuatilia kwa karibu miradi ya maendeleo iliyo katika maeneo yao kwani baadhi ya wakandarasi pamoja na kupewa malipo ya awali lakini hawawendi kufanya kazi walizoomba.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato