Na Esther Macha,timesmajira,Online,Mbeya
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Mbeya imefanikiwa kuwabana wadaiwa sugu wanaodaiwa na kuokoa zaidi ya sh. 405,626,605.
Taasisi zilizobanwa ni pamoja na vyama vya ushirika (AMCOS),vyama vya kuweka na kukopa, Halmashauri, taasisi mbalimbali zinazohusika na ukusanyaji wa kodi za Serikali.
Hata hivyo imeelezwa kuwa TAKUKURU ilifanya ufuatiliaji wa fedha hizo katika wilaya zote za mkoa wa Mbeya na kufanikiwa kurejesha fedha hizo.
Hayo yalisemwa jana na Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mbeya, Abdaudi Mbura wakati akitoa taarifa ya miezi mitatu ya utendaji wa waandishi hiyo kwa wanahabari.
Mbura alisema kiashi cha sh. 205,379,805 ziliokolewa kutoka kwa watumishi ambao walipewa jukumu la kukusanya mapato kupitia mashine za kielektroniki na hawakuwasilishwa mapato waliyokusanya kwa wakati katika halmashauri zao.
Hata hivyo Mbura Naibu alisema shilingi milioni .10 ziliokolewa kutoka Kwa Diwani aliyemaliza muda wake ambayo ilikabidhiwa kwake kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Amos makala iliyopo wilayani Chunya na kuichukua kama mali yake binafsi.
“Lakini pia kuna shilingi milioni 177,175,330 ziliokolewa kutoka kwenye vyama vya ushirika ambazo ni fedha zilizofujwa na viongozi wa vyama na mikopo ambazo zilikuwa hazijarejeshwa na wanachama waliokopa.
Pia akieleza zaidi alisema sh.880,000 ziliokolewa kutoka kwa vikundi mbali mbali vilivyokuwa vimekopeshwa na halmashauri kutoka katika fungu la asilimia 10 la mapato ya ndani.
Alisema kwamba sh. 6,191,470 ni fedha zilizokoolewa kutoka katika sekta za ujenzi,mabaraza ya kata, ardhi na binafsi.
Akizungumzia kuhusu uchunguzi wa mashtaka yalifanyiwa kazi na TAKUKURU, Mbura alisema katika kipindi cha Aprili hadi Juni jumla taarifa 137 za tuhuma za rushwa na makosa mengine zilifanyiwa uchunguzi na taasisi hiyo.
Aidha Mbura alisema katika kipindi hicho TAKUKURU iliendelesha na kesi zilizokuwa mahakamani na kuweza kufungua kesi mpya tano na kushinda kesi nne na kushindwa kesi moja.
More Stories
Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi
Rais Samia apongezwa kwa kuboresha huduma kwa wazee
Watu 5,000 kuhudhuria tamasha la utamaduni Songea