Na Israel Mwaisaka, Timesmajira Online -Rukwa
Mkurugenzi Mkuu wa Taaisisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU),nchini Crispin Chalamila,amewahimiza wananchi kutumia haki yao ya kikatiba kushiriki kwenye uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025 ili kuchagua viongozi sahihi.
Chalamila ametoa wito huo wakati wa uzinduzi wa jengo la utawala la TAKUKURU wilayani Nkasi,lililogharimu zaidi ya shilingi millioni 300,na kusisisitiza jamii umuhimu wa ushiriki kwenye uchaguzi mkuu kwa kujitokeza kupiga kura kwa maendeleo ya taifa.

Amesema uwepo wa jengo hilo utasaidia kuongeza ufanisi na kuboresha huduma katika mapambano dhidi ya rushwa huku akiwataka watumishi wa taasisi hiyo kulitunza jengo hilo ili liweze kudumu kwa muda mrefu na kuleta tija katika maeneo husika.
Pia amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU kwa kufichua vitendo vya rushwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miliki kutoka TAKUKURU Mhandisi Emmanuel Kiyabo,amesema uwepo wa majengo hayo ni mwanzo mzuri kwa taasisi hiyo katika utoaji na uboreshaji wa huduma kwa wananchi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nkasi,Peter Lijualikali,amewataka TAKUKURU kuongeza jitihada katika mapambano dhidi ya rushwa, wao kama viongozi wapo tayari kutoa ushirikiano katika taasisi hiyo ili kuweza kuyafikia malengo husika.
Hata hivyo TAKUKURU nchini ina upungufu wa mjengo 64 ambapo hadi kufikia mwaka 2025 majengo 70 yamejengwa na kuanza kutoa huduma.


More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako