
Na Moses Ng’wat, Mbozi.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Songwe, imeandaa hafla ya futari kwa viongozi wa dini, watoto, watu wenye uhitaji, pamoja na wananchi, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mshikamano na ushirikiano kati ya taasisi hiyo na jamii.
Hafla hiyo, iliyofanyika Machi 17, 2026, katika Ukumbi wa Chiku Galawa, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe, ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Hamad Mbega, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa, ambaye alikuwa mgeni rasmi.

Akizungumza katika tukio hilo, Dc Mbega alisema kuwa utoaji wa futari ni ishara ya mshikamano, upendo, na kujali makundi mbalimbali ya jamii, hususan yatima na viongozi wa dini.
Aliongeza kuwa makundi hayo yamekuwa mstari wa mbele kuhimiza maadili mema na amani katika jamii..

Kwa upande wake, Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Songwe, Frida Wikesi, aliwashukuru wote waliohudhuria hafla hiyo, huku akitumia fursa hiyo kuomba jamii kuisaidia taasisi hiyo kufichua vitendo vya rushwa.



More Stories
JNHPP: Ndoto ya Nyerere yatimia,Rais Samia apongezwa
Rais Samia aagiza wakuu wa Mikoa kujiandaa na udhibiti wa Athari za El Nino
InnoIP Tanzania yazinduliwa kuimarisha ulinzi wa ubunifu