November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TAKUKURU Mwanza yatupia macho miradi ya maendeleo ya thamani ya bilioni 6.1

Na Daud Magesa, Timesmajira Online, Mwanza

MIRADI saba ya maendeleo inayotekelezwa kwa gharama ya bilioni 6.1 kati ya 15 yenye thamani ya bilioni 19.11, inachunguzwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU),mkoani Mwanza kutokana na mapungufu mbalimbali.

Ambapo taasisi hiyo imeiwezesha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), mkoani humo kukusanya kiasi milioni 68.1 za kodi ya zuio na kuleta matokeo chanya baada ya kuchambua mfumo wa mapato ya kodi hiyo katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.

Akizungumza Aprili 29,2024 na waandishi wa habari, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza,James Ruge,amesema miradi hiyo ni ya sekta za afya, elimu, maji, uchukuzi na utawala,iliofuatiliwa na kukaguliwa katika kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu ili kufahamu ubora na thamani ya fedha zilizotumika.

“Miradi hiyo 15 iliyokaguliwa, saba ilikutwa na mapungufu ya kutokamilika kwa wakati ukiwemo wa jengo la utawala la Halmashauri ya Kwimba ambao mkataba umevunjwa,ukarabati wa lambo la maji ya kunyeshwa mifugo Nyambiti,vifaa vya ujenzi viliharibika sababu ya utunzaji mbovu na vingine viliibwa,”amesema Ruge.

Amesema miradi mitatu ya maji ya matokeo ya haraka wilayani Nyamagana,nyaraka za malipo ya awali,nyaraka za kodi ya VAT na kodi ya zuio, halikuwasilishwa kwa ajili ya uhakiki huku miradi ya ukarabati wa barabara ya Km 4 ya Usagara-jijini Mwanza pamoja na barabara ya Bukumbi Hospitali ya urefu wa Km 2, wilayani Misungwi mitaro yake ilibomolewa na mvua kabla ya mradi kukabidhiwa.

Mkuu huyo TAKUKURU amesema majalada ya uchunguzi yamefunguliwa na unaendelea kwa miradi saba iliyobainika kuwa na mapungufu makubwa ukiwemo ujenzi wa nyumba pacha ya walimu katika shule ya sekondari Buzuruga iliyojengwa katika kiwanja cha Esther Mtaki.

Pia kazi hiyo ya uchambuzi wa mfumo wa mapato ya kodi ya zuio imesaidia kutambuliwa kwa taasisi 37 katika Wilaya ya Kwimba,11 kati ya hizo zimesajiliwa na kupewa namba ya mlipa kodi (TIN),ili zilipe kodi hiyo kwa mujibu wa sheria.

Ruge amesema mafanikio hayo yametokana na maazimio yaliyowekwa na TAKUKURU ya namna bora ya kukusanya kodi ya zuio baada ya uchambuzi wa mfumo kufanyika ambapo mapungufu mbalimbali yalibainika ikiwemo halmashauri kutokusanya kodi hiyo.

Pia uelewa mdogo wa kodi ya zuio kwa wafanyabiashara na watoa huduma baadhi hasa mafundi ujenzi (local) kutokuwa na TIN.

“Moja ya majukumu ya TAKUKURU kudhibiti mianya ya rushwa kwa kuchambua mifumo ya utendaji kazi katika taasisi za umma na zisizo za kiserikali,ili kubaini mianya hiyo ya rushwa na hatimaye kushauri namna bora ya kutoa huduma na kuepuka vitendo vya rushwa,”amesema.

Aidha ameeleza kuwa katika kipindi hicho cha Januari hadi Mwachi, 2024 ,kwa kazi za uchunguzi walipokea taarifa 70 kati ya hizo 44 za vitendo vya rushwa na 26 hazikuhusiana na vitendo hivyo na uchunguzi uko hatua mbalimbali.

Ameongeza kuwa,taarifa 18 wahusika walishauriwa,tano zilifungwa, moja ilihamishiwa idara nyingine na mbili zinafuatiliwa huku upande wa mashitaka mashauri yaliyokuwa mahakamani, Jamhuri ilishinda kesi tano kati ya 33 ambapo kesi 28 zinaendelea kusikilizwa .

Aidha, katika kipindi hicho makundi mbalimbali ya wananchi yalielimishwa madhara na makosa ya rushwa pamoja na wajibu wao wa kushiriki kuzuia na kupambana na rushwa ambapo semina 71 zilifanyika kwa watumishi wa sekta za umma na binafsi.

Pia mikutano 56 ya hadhara kwa wananchi ilifanyika katika kata na mitaa,kuimarisha klabu za wapinga rushwa katika shule za msingi, sekondari na vyuo,uandishi wa habari zenye ujumbe wa kuelimisha jamii na kukemea vitendo vya rushwa ziliandikwa,vipindi vitano vya redio vilirushwa na maonesho 10 yalif