November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TAKUKURU kinondoni yabaini mapungufu machache katika utakelezaji wa miradi ya maendeleo

Na Mwandishi wetu, Timesmajira online

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKUKU )Mkoa wa Kinondoni imesema katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Septemba mwaka huu imebaini mapungufu machache katika utekelezaji wa miradi ya Maendeleo katika Halmshauri ya Manispaa ya Ubungo na Kinondoni.

Mapungufu hayo yameonekana katika mfumo wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kieletroniki PSO Mashine pamoja na mfumo wa huduma za maji kutoka Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira Dar es salaam (DAWASA)

Akitoa taarifa ya Utendaji kazi kwa kipindi cha Julai hadi Septemba 2024 Kaimu Mkuu wa TAKUKUKU Mkoa wa Kinondoni, Christian Nyakizee amesema
katika kipindi husika wameweza kufuatilia miradi sita yenye thamani Billioni 15, 982,221, 355.9 ambayo inaendelea na utekelezaji.

” Tumebaini mapungufu machache katika ambayo wahusika wameshauriwa kurekebisha mapungufu hayo na tunaendelea kufuatilia kwa karibu hadi miradi itakapokamilika ili kuhakikisha inakuwa na ubora na kwa kuzingatia thamani ya fedha”amesema Nyakizee

Kwa upande mfumo wa ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kieletroniki Nyakizee amesema wamebaini wakusanya mapato wengi waliokuwa wanatumia mashine hizo za kieletroniki PSO mashine kutokuzingatia sheria na taratibu ambazo zipo kwenye mkataba waliosaini.

“TAKUKUKU imefanya uchambuzi wa mfumo wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kieletroniki PSO katika Halmshauri ya Ubungo na kubaini wakusanya mapato wanaotumia Mashine za PSO awazingatii Sheria na taratibu zilizopo katika mkataba waliosaini kati yao na Mkurugenzi wa Halmshauri ya Manispaa ya Ubungo “amesema Nyakizee

Vilevile amesema kwa upande wa utoaji wa huduma za maji DAWASA katika Halmshauri ya Manispaa ya Kinondoni wamebaini kuwepo kwa chagamoto katika utekelezaji wa ankra unaotokana na uwepo wa dira za maji ndani ya makazi ya wateja.

Amesem hali hiyo ilipelekea ucheleweshaji kwenye usomaji dira kutokana na kutokufikia dira kwa wakati huku baadhi ya dira kuwa na ukungu na kupelekea kusoma usomaji usio sahihi .

“Mfumo wa Ankra yaani MAJIIS unaosimamiwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGa) hukumbwa na chagamoto za mtandao kipindi cha zoezi la usomaji dira na kukosekana kwa ushirikiano kutoka kwa baadhi ya wateja kipindi cha usomaji dira”amesema Nyakizee

Kaimu Mkuu huyo wa TAKUKUKU Kinondoni aliendelea kueleza kuwa Taasisi hiyo imepokea jumla ya malalamiko 104 ambayo kati ya hayo 72 yalihusu rushwa na 32 yasiyohusu rushwa.

Amesema malalamiko ambayo hayakuhusu rushwa walalamikaji wengine wameshauriwa na majalada kufungwa na wengine wameelekezwa sehemu sahihi ya kupelekea malalamiko yao.

Pia aliongeza kuwa TAKUKUKU Kinondoni imefungua mashauri mapya mawili katika mahakama ya wilaya ya Ubungo huku mashauri saba yakitolewa maamuzi na Jamhuri na kushinda mashauri matatu na 24 yakiendelea mahakamani.

Aidha amesema katika kuelekea Uchaguzi wa Serikali za mtaa TAKUKUKU Kinondoni imejipanga kuendelea kuelimisha wananchi wajue madhara ya rushwa na wahamasike kushirikiana na Taasisi hiyo kutokomeza rushwa .

“Rushwa katika Uchaguzi upelekea kuchaguliwa kwa viongozi wasio waadilifu watakaotumia muda wao mwingi wa uongozi kurejesha fedha zao na sio kuleta maendeleo kwa wananchi”alisisitiza Nyakizee

Pia ametoa wito kwa wananchi wote katika Mkoa huo kuendelea kutoa ushirikiano kwa TAKUKUKU Kinondoni na kuwasihi kuwa wapatapo taarifa zozote za rushwa wawasiliane nao kwa kupiga na kutumia ujumbe mfupi kwa namba 113.