Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Ilala, (TAKUKURU)wametoa mafunzo kwa Walimu wa shule za Msingi na Sekondari wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kuwajengea uwezo kwani Walimu ni wasimamizi Wakuu wa miradi ya Serikali.
Hayo yalisemwa na Afisa TAKUKURU mkoa Ilala Sosthenes Kibwengo ,wakati wa mafunzo ya walimu wa Wilaya ya Ilala ambayo yanawashirikisha shule za Serikali na shule Binafsi.
“Serikali inataka kujenga kizazi cha WAZALENDO wasifuate Rushwa na walimu wapo shule za msingi na sekondari walezi wa vijana hivyo vijana wakipata elimu hiyo shuleni Serikali itapata Taifa bora WAZALENDO”alisema Kibwengo .
Mkuu wa TAKUKURU Ilala Kibwengo alisema pia walimu wanasimamia miradi ya Serikali na wengine maafisa ununuzi hivyo mafunzo hayo yatawasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao mbali mbali katika kazi za Serikali
Alisema klabu za rushwa zinatakiwa ziwe na wanachama wengi walimu ni walezi na chachu katika shule kutoa elimu.
Aidha alisema wazazi inawategemea Walimu na Serikali walimu wakipata elimu hiyo itawasaidia kupambana na Rushwa.
Alisema mafunzo hayo kwa walimu watatoka na maazimio sahihi ikiwemo wanafunzi wasome kwa bidii na kuchukia Rushwa.
Akizungumzia mikakati ya TAKUKURU mkoa wa Ilala kampeni ya madawa ya kulevya na kuwataka vijana wachukue hatua madawa ya kulevya yana hasara kubwa kwa Taifa kwa jamii na kizazi
Aliwataka wanachama wengine wajiunge na klabu hizo mashuleni waweze kuchukia rushwa kuwa kioo cha jamii kwa uzalendo wa nchi yao.
Pia aliwataka wajumbe manunuzi na wajumbe wa Kamati za Ujenzi shuleni wazingatie mafunzo hayo wawe kioo cha jamii na wasimamizi wa miradi ya Serikali wawe wasimamizi wazuri.
Alisema TAKUKURU Ilala inawataka Walimu wazingatie sheria ,kanuni na taratibu wasitumie rushwa kwani rushwa ni adui wa haki wakatae rushwa kwa vitendo wafuate sheria na kanuni za nchi.
Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Asha Mapunda, alimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Jamary Mrisho Satura kwa mafunzo hayo kwa walimu wa Wilaya ya Ilala ambayo yamewashirikisha shule za Sekondari, shule za Msingi zote za Serikali pamoja na shule Binafsi zilizopo wilaya Ilala.
Afisa Elimu Asha Mapunda alisema dhumuni la mafunzo hayo Serikali ya Wilaya Ilala mikakati yake ijenge kizazi bora rushwa ni adui wa haki .
“Walimu wanaenda fundisha wanafunzi wetu na Taifa la baadae hivyo watakuwa viongozi bora wa kesho watakaojenga Taifa letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania “alisema Asha
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi