Na Irene Clemence, TimesMajira Online, DSM
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Mkoa wa Ilala imesema imejipanga kufuatilia mchakato mzima wa Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
Akizungumza na waadishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana wakati akitoa taarifa ya TAKUKURU Mkoa wa Ilala kwa kipindi cha miezi mitatu, Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Ilala, Elizabeth Mokiwa amesema Taasisi hiyo imejipanga kuchukua stahiki ili kuhakikisha vitendo vya rushwa vinazibitiwa.
Amesema vitendo vya rushwa vitadhibitiwa kabla, wakati na baada ya uchaguzi Mkuu.
“TAKUKURU Mkoa wa Ilala tunajukumu la kufuatilia na kuhakikisha wagombea wote wanaojiusisha na vitendo vya rushwa katika mchakato wa uchaguzi wanabainika”amesema Mokiwa.
Alibainisha kuwa katika kipindi cha Julai hadi Septemba wamejipanga kufanya mikutano ya hadhara kwa lengo la kuwapatia wananchi elimu ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa katika kuelekea uchaguzi mkuu.
“Kama mnavofahamu mwaka huu tunazoezi la uchaguzi mkuu mwezi Oktoba hivyo wananchi watapata elimu ya Kupambana na vitendo vya rushwa mapema”amesema Mokiwa.
Aidha amesema katika kipindi cha Aprili hadi Juni mwaka huu taasisi hiyo imefungua kesi mpya tano huku mashauri 22 yakiendelea mahakamani .
More Stories
Bei za mafuta Novemba 2024,zaendelea Kushuka
TARURA yaomba Mkandarasi aitwe
Ilemela yakusanya bilioni 3.7.robo ya kwanza