October 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Aliyekuwa Mbunge wa Mtera CCM Livinhstone Lusinde (Kibajaji) akizungumza na waandishi wa habari jijijini Dodoma . Picha na Joyce Kasiki, TimesMajira Online, Dodoma

Takukuru Dodoma yamsafisha Lusinde (Kibajaji)

Joyce Kasiki, TimesMajira Online, Dodoma

MKUU wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani wa Dodoma, Sostenes Kibwengo amesema,taasisi hiyo haitaendelea na kesi ya tuhuma za rushwa ya aliyekuwa Mbunge wa Mtera kupitia CCM, Livingstone Lusinde (Kibajaji) kutokana na kukosekana uthibitisho wowote.

Kibwengo ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma.

Kibwengo amesema kuwa hadi sasa taasisi hiyo bado haijapata uthibitisho wowote wa Mbunge huyo kuwa alitoa rushwa kwa wajumbe ili wamsaidie katika mchakato wa uchaguzi Mkuu ujao.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Lusinde amesema kuwa yeye hakutoa rushwa, bali aliyetoa taarifa hiyo alikuwa na lengo la kumchafua
kisiasa.

“Pale kwangu nilikuwa na shughuli ya mjukuu wangu kwa hiyo nilikuwa na wageni wengi,mtu akatumia nafasi hiyo kunichafua na kutoa
taarifa takukuru kuwa nilikuwa natoa rushwa kwa wajumbe.

“Jambo hili siyo kweli maana mimi mwenyewe najiamini ni msafi na ndio maana namshukuru Mungu kwamba walinizushia, lakini Takukuru wamechunguza wamebaini kuwa sikuhusika kutoa rushwa,sasa niwaambie tu kwamba wamefeli na wasiyempenda kaja,” amesema Lusinde na kuongeza kuwa;

“Tena naomba watambue kuwa ng’ombe mwenye mimba huwa hachinjwi” Lusinde ametoa rai kwa watoa taarifa kuhakikisha wanatoa
taarifa kwa mamlaka husika ambazo zina uhakika .

Hivi karibuni Taasisi hiyo ilimshikilia Lusinde na kumfanyia mahojiano baada ya kuoata taarifa za viashiria vya rushwa nyumbani kwake.