March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TAJU kufanya maombi maalum dhidi ya Uchaguzi Mkuu

Na Bakari Lulela,Timesmajira

TAASISI ya watu wenye Ulemavu nchini TAJU imetoa wito kwa watanzania wa ngazi mbalimbali kujitokeza kushiriki uchaguzi mkuu kwa kuzingatia amani,upendo  utulivu na mshikamano ndani ya jamii yetu.

Uchaguzi huo unatarajia kufanyika mwezi octoba 29, ,2025 nchini kote Tanzania Jumuishi wanatoa tamko kwa kuzingatia kauli mbiu yao Tupange wote, tutekeleze wote na tutathmini wote kwenye kila jambo linalohusu jamii ya watanzania.

Akizungumza jijini Dar es salaam kwenye hafla fupi ya kuuombea amani uchaguzi mkuu wa Tanzania Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Ndonge Said Ndonge amesema kwamba chaguzi mara nyingine zimekuwa ni chanzo cha vurugu na uvunjifu wa amani, siyo tu Tanzania Bali pia katika mataifa mengi.

“Kwa kutambua hilo TAJU kwa nia nzuri kabida na ya kizalendo imeonelea kuliongelea Hilo Ili kuuombea amani uchaguzi mkuu Ili nchi iendelee kuwa kisiwa cha amani na salama kwa kila mtanzania wakiwemo watu wenye Ulemavu,” amesema Ndonge

Aidha Mwenyekiti ameeleza kwamba mara nyingine kumekuwa na Dhana inayodai kwamba, penye machafuko ya kisasa na uvunjifu wa amani wanaoathirika zaidi ni akina mama na watoto Dhana hii ni sahihi na Haina kasoro yeyote ambapo TAJU inaikubali Dhana hii mia kwa mia na kudai kuwa Kuna kundi ambalo linaloathirika zaidi lakini limesahauliwa ndio maana taasisi hii inalisemea.

Kwa upande wake Katibu mkuu wa TAJU Taifa Innocent Gabriel amesema kuwa sauti za watu wenye Ulemavu ni sehemu ya jamii hivyo inatoa wito wa kushiriki kwa umoja na nguvu kuwapigia kura viongozi watakao liongoza Taifa la watanzania.

Hata hivyo panapojitokeza matatizo ya uvunjifu wa amani watu wenye Ulemavu, akina mama na watoto huathirika zaidi kwa kuwa kundi hili wengi wao hawawezi kukimbia na vurugu hizo huwa ni chanzo cha kifo ama kupata madhara zaidi, kwa mantiki hii kundi la watu wenye Ulemavu linahitaji amani zaidi kuliko kundi lolote ndani ya jamii.

Nae mratibu wa dawati la watu wenye Ulemavu Emanuel Majeshi amesema kuwa Ili uchaguzi huo uwe wa haki na amani kwanza tunawaomba viongozi na wasimamizi wa uchaguzi watende haki ili kila mshiriki kwenye uchaguzi aridhike na mchakato na matokeo ya uchaguzi.

Mkuu huyo amesema kuwa wanawaomba washiriki wote wa uchaguzi kwa maana ya wagombea wa ngazi mbalimbali na vyama vya siasa wazingatie Sheria  zilizopo Ili kujiepusha na vitendo vya vurugu na uvunjifu wa Sheria. Ambapo wanawaomba viongozi wa dini zote kwa pamoja wasaidie kuliombea Taifa kwa kufanya sala za maombi  ya amani