January 13, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Taifa Stars kulamba Mil 500/= ikifuzu Afcon

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Serikali itatoa kiasi cha Shilingi Milioni 500 endapo timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) itafuzu kushiriki Fainali za Kombe la Mataifa Barani Afrika (AFCON) mwaka 2024 nchini Ivory Coast.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam ambapo amesema Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Hamis Mwinjuma ataongoza Watanzania wa hapa nchini na waishio nchini Misri kuishangilia Taifa Stars.

“Nawaomba Watanzania tujitokeze kwa wingi kuishangilia Taifa Stars katika mchezo wetu utkaochezwa machi 24 mwaka huu, dhidi ya Uganda (The Cranes) utakaochezwa katika mji wa Isimailia nchini Misri na mchezo wa marudiano utachezwa Machi 28, Uwanja wa Benjamini Mkapa,” amesema Balozi Dkt Chana.

Aidha, amewataka wadau wa mchezo huo ikiwemo Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na mashabiki kumuunga mkono Kocha wa Timu hiyo Adel Amrouche, huku akiwasistiza wachezaji wajitume ili waweze kufanya vizuri katika nashindano hayo.