Na Queen Lema, Timesmajira Online,Arusha
Wito umetolewa Kwa taasisi Za fedha nchini hapa kubuni mbinu na teknolojia mbadala za kuwasaidia watu wenye ulemavu,pindi watakapoitaji huduma ndani ya taasisi hizo
Kwani kwa sasa hakuna teknolojia mbadala ambayo inaweza kuwasaidia walemavu mbalimbali kuweza kupata huduma katika taasisi hizo hasa benki.
Hayo yameelezwa na Renatus Rupoli wakati akichangia mada katika mkutano wa Asasi za Kiraia (Azaki) unaoendelea jijini Arusha.
Amesema kuwa walemavu hasa wa macho wakati mwingine wanashindwa kutumia huduma kama za ATM kwa saba hawawezi kutambua lakini sasa ni muhimu kwa benki nchini hapa kufikiria suala hilo.
“walemavu hasa wa macho wakati mwingine wanapata shida kubwa na wanakosa haki zao za msingi, kwanini msije na teknolojia ambayo sasa itaweza kutusaidia huku taifa likipata maslahi,”amesema Rupoli.
Akizungumzia suala hilo kama mdau wa huduma za kifedha Amali Bazanzali kutoka benki ya Stanbic amesema kuwa ni kweli changamoto hiyo ipo na siyo kwa benki hiyo tu bali kwa benki nyingi nchini hapa.
Amali amesema kuwa wanafanyia kazi sulala hilo kwa kuwa teknolojia imekuwa na wataona namna ya kuja na mbinu mbadala za kuwasaidia walemavu hasa wa macho.
Mkutano huo unaoendelea jijini Arusha umeweza kuwakutanisha wadau kutoka maeneo mbalimbali nchini pamoja na nje ya nchi huku suala zima la teknolojia likiwa linaangaziwa katika sekta mbalimbali.
More Stories
Kamati ya Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini yagawa vifaa vya ujenzi
Hatma mrithi wa Kinana kupatikana
Mrithi wa Kinana CCM kujulikana katika Mkutano Mkuu wa Jan 18/19