December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Taasisi ya Sambaza upendo yawasaidia wenye uhitaji Dar

Na Bakari Lulela, Timesmajira Online

IMEELEZWA kuwa utajiri wa nafasi ni jambo jema katika kuwaonea huruma viumbe wa mungu hivyo Ibada na kumtegemea yeye ni msingi wa maisha  Bora ya hapa duniani na kesho akhera.

Hayo yamebaishwa  jijini katika msikiti wa Shia ith na Sheria kigogo Dar es salaam, na sheikh Ahmed Abdi ambaye alisisimama baada ya kukosekana mkuu wa wilaya ya ubungo ambaye ndiye aliyepangwa kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo sheikh Ahmed amesema kufanya mambo mema pamoja na kuwaonea huruma viumbe wa mungu ni mambo yanayompendeza mungu.

“Mtume wetu Muhammad (saw) hajasifiwa kwa kusali bali alisifiwa kwa kuwasaidia watu waliomzunguka na wenye itikadi mbalimbali ikiwemo waislamu na wakristo pamoja na wasiokuwa na dini,” amesema sheikh Abdi

Aidha sheikh Abdi amesema UMOJA wanaouonesha taasisi ya sambaza upendo ni kioo kwa jamii katika kuwasaidia watu wanaoishi katika mazingira magumu, wajane, mayatima yanapaswa kuigwa na kila mmoja wetu.

Kwa upande wa risala kutoka kikundi cha sambaza upendo iliyosomwa na Askofu Mary Mudirikati imesema mbali na kusaidia makundi ya wahitaji wamekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhitaji wa eneo kwa ajili ya kujenga kituo cha watoto, sehemu ya kufungua viwanda vidogovidogo na usafiri wa kuwafikia na kueneza upendo na amani ndani ya jamii.

Nae kiongozi wa msikiti huo sheikh Said Athuman amesema kuwa kila mwenye neema atakusudiwa na mungu hivyo kila kiumbe anapaswa kuishi kwa amani na upendo isitoshe walioshinda katika maisha ya Dunia ni wale walioshinda matamanio yao.

Pia kiongozi wa Sambaza upendo askofu Amani Kayuni ameeleza kuwa siku zote UMOJA hutengeneza mshikamano na mshikamano hutengeneza UMOJA kati ya waislamu na wakristo hivyo wote ni kitu kimoja katika kuitunza amani yetu na upendo utaweza kuthibitika.

Katika hafla hiyo Sambaza upendo, amani na UMOJA ilihudhuriwa na waumini tofauti ambapo ilitolewa misaada mbalimbali kwa makundi maalumu ya wahitaji ikiwemo wazee wanaoishi katika mazingira magumu, wajane na yatima