Na Penina Malundo, TimesMajira Online
TAASISI ya Lukiza Autism imekabidhi hundi ya kiasi cha Sh. Milioni 4.1 kwa kituo cha ufundi cha Watoto wenye Changamoto za Ufahamu cha Salt kilichopo Mbezi Makabe jijini Dar es Salaam, ikiwa ni moja ya madhumuni ya mbio za hisani (Run 4 Autism inclusive Marathon 2022) Â zilizofanyika Aprili 10,2022.
Pia wametoa medari kwa waandishi wa habari katika kutambua mchango wao katika kuandika habari za watu wenye ulemavu hususani kwa walemavu wenye tatizo la usonji .
Msaada huo  umekabidhiwa leo jijini humo na Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa  Taasisi ya Lukiza Autism,Hilda Nkabe alisema msaada huu ni moja
ya utekelezaji wa malengo ya taasisi yake ya kuwawezesha vijana wenye Usonji na Ulemavu mwingine kupata ujuzi wa kilimo mahiri ili kuja kuweza kujipatia chakula na pia kujishughulisha kwenye shughuli
za Kiuchumi.
Amesema mradi huo wa Kilimo na Ufungaji wa Kuku na Samaki kwa vijana hao utawawezesha kwa kiasi kikubwa kupata mboga na Chakula hata fedha za kujikimu katika kituo hicho pindi watakapopata Chakula cha ziada na kuja kukiuza.
“Fedha hizi tulizipata katika mbio tulizozifanya za kuelimisha jamii kuhusu usonji ilikuwa ni uadhimisha wa mwezi wa kuelimisha jamii kuhusu Usonji Duniani, Kuelimisha jamii juu ya ujumuishwaji wa watu wenye changamoto ya Usonji katika shughuli zote za afya,
elimu, kiuchumi na kijamii,Kuwakutanisha wazazi, walezi, wadau na mashirika yasiyo ya kiserikali, wanahabari, watunga sera na wananchi wote kwa ujumla ili kuweza kubaini changamoto na fursa kwa vijana na watoto
wenye changamoto ya usonji pamoja na changamoto zingine za ufahamu,”amesema na kuongeza
“Pia kuhamasisha familia zenye watoto
wenye Usonji na ulemavu mwingine kutowaficha watoto wao ,tumefanikiwa haya na la mwisho lilikuwa hili la kuchangisha pesa za kusaidia kituo
cha ufundi cha SALT, nalo tumelikamilisha,”amesema
Nkabe amesema kituo hicho cha Salt kinahudumia watoto wenye ulemavu wa ufahamu kama watoto wenye sura mfanano(down syndrome), mtindio
wa ubongo, kupooza ubongo, Usonji na kifafa kikali.
“Manufaa ya mradi huu ni makubwa sana kwa vijana wa kituo hiki kwani watoto wanalala hapa hapa hivyo wataweza kufanya shughuli zao wenyewe na kujipatia Chakula kupitia mradi huo na mradi ukiendelea vizuri na kupata mazao ya ziada wataweza kuuza ili kupata fedha ambazo zitawasaidia katika matumizi mbalimbali ya ndani ya kituo,”amesema Nkabe
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa kituo cha Salt, Rebecca Lebi, amesema fedha hizo zitatumika kuendeleza mradi wa kilimo mahili
cha mjini (intensive urban farming) ambapo utajumuisha ufugaji wa samaki kwa njia ya matanki, kilimo cha mbogamboga kwa matone na ufugaji wa kuku wa kienyeji.
Amesema fedha hizo zitasaidia mradi huu kuanza mara moja
kwa kununulia vifaa na pembejeo, kuwezesha kupata mbogamboga, kuku na samaki salama kwa ajili ya matumizi ya kituo na pia kuweza kuuza kwa madhumini ya kujipatia fedha kwa matumizi ya kituo kama kulipia
bili za maji na umeme.
” Tunawashukuru wadau wote waliowezesha kufanikisha mbio hizi na kuweza kukamilisha malengo yetu,tunatoa wito kwa wadau mbalimbali na wafadhili kuunga mkono juhudi za taasisi Lukiza Autism na mbio za Run 4 Autism Tanzania,”amesema
More Stories
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best
Waziri Mavunde:Benki Kuu yanunua tani 2.6 za Dhahabu nchini