May 3, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Taarifa za mfumo wa anwani za makazi kutumika kwenye mawasiliano

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bwn. Kaspar Mmuya ameshauri watendaji kuanza kutumia taarifa za mfumo wa Anwani za makazi Postikodi kwenye barua za ofisi ili kurahisha mawasiliano kwa watu kujua eneo zinapopatikana Ofisi

“Watendaji tuanze kujitambulisha kwenye mikutano kwa mfumo wa Anwani za makazi ili kutoa hamasa zaidi kwa wananchi alisema Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu”

Naibu Katibu Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu ametoa ushauri huo leo tarehe 19/05/2022 Katika ziara yake ya kikazi Mkoani Pwani Halmashauri ya Kibaha Mji, alipoenda kujionea utekelezaji wa Operesheni Anwani za makazi.

Afisa Mtendaji mtaa wa mkoani A Kibaha Bwn. Jakson Mwakalima amesema tayari wameshapata mtengenezaji wa vibao vya nyumba, ambavyo mwananchi anaenda kununua kwa shilingi elfu Mbili na kubandika kwenye nyumba yake.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bwn. Kaspar Mmuya akizungumza na watendaji (ambao hawapo kwenye picha) katika Ofisi ya Mtendaji, Kata Matumbi kukagua utekelezaji wa operesheni ya Anwani za makazi Halmashauri ya Mji wa Kibaha.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bwn. Kaspar Mmuya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Bi,Optuna Kitanda na watendaji wakitazama vibao vya nyumba vilivyoandaliwa tayari kwa kubandikwa kwenye nyumba katika ziara yake kata ya Tumbi Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Pwani.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bwn. Kaspar Mmuya akitoa maelekezo kwa Watendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Mji, mara baada ya kukagua utekelezaji wa Operesheni Anwani za Makazi katika Halmashauri ya Mji huo.