November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

T-PESA kutumia wiki ya huduma za fedha kuelimisha vijana fursa za ajira


Na Rose Itono

KAMPUNI Tanzu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania, T-PESA Imeendelea kutumia maadhimidho ya
wiki ya huduma za fedha kwa kuwapatia elimu wateja wake na wananchi Ili waweze kuzifahamu huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo sambamba na fursa zinazoweza kupatikana kwa vijana katika kujikwamua kiuchumi

Akitoa taarifa kwa vyombo Vya habari Ofisa Uhusiano wa TTCL
Adeline Berchimance amesema Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha yanayofanyika katika Viwanja vya Shekhe Amri Abeid jijini Arusha.yameandaliwa na Wizara ya Fedha na kuzishirikisha Taasisi ndogo za fedha, yamelenga kuwajengea uelewa kuhusu matunizi sahihi ya fedha mtandao
na fursa nyingine mbalimbali za kifedha

“Maadhimisho ya wiki ya huduma za fedha yaliyoandallwa na Wizara ya Fedha yamezishirikisha
Taasisi ndogo za fedha,
Mabenki, Mifuko ya Hifadhi za Jamii pamoja na wajasiriamali kwa lengo la kukutanisha Kampuni ya T-PESA na Wananchi Ili kuwajengea uelewa kuhusu matumizi sahihi ya fedha mtandao na fursa mbalimbali zinazopatikana katika Kampuni hiyo na namna zinavyoweza kuwasaidia kujikwamua kiuchumi,” amesema Berchimance

Amesema katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kutatua changamoto za ajira kwa vijana T-PESA inayofursa mbalimbali kwa vijana zitakazosaidia kujitengenezea kipato na hivyo kujikwamua kiuchumi.

“T-PESA inazo fursa mbalimbali hasa kwa vijana ikiwa ni pamoja na uwakala ambapo wanaweza kufanya biashara hii ya kuwa Wakala na kujipatia kipato cha kusaidia familia zao kwani T-PESA tunatoa kamisheni kubwa zaidi ukilinganisha na mitandao mingine” amesema Berchimance

Aidha amesema Maadhimisho hayo pamoja na mambo mengine yametoa fursa kwa Kampuni hiyo kukutana na Wateja na Wananchi kwa ukubwa zaidi na kujibu hoja, maswali na kero zao na hivyo maadhimisho hayo yamekuwa muhimu katika kupata mrejesho sahihi kuhusu huduma na bidhaa zinazotolewa na T-PESA.

Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yamefanyika kwa mara ya tatu Mkoani Arusha na kwa mwaka huu yalikuwa na kauli mbiu isemayo Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi.

Maadhimidho hayo yamezinduliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali.